Hizi Ndio Siasa Zetu

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
233
Hakuna mchezo mzuri kama mchezo unaoitwa SIASA katika siasa utaona maajabu mengi sana na mambo mengi sana ambayo huwezi kufikiria kama yanaweza kutokea au angalau kusemwa na watu wenye hadhi zao na watu ambao maisha yao yote wametumikia mataifa yao kwa moyo mmoja na uzalendo wa hali ya juu .

Lakini kuna mambo ambayo mimi napenda nasiingizwe katika siasa haswa mambo yenye masilahi kwa nchi yetu , mambo ambayo kila mwananchi anatakiwa achangie chochote alichokuwa na uwezo nacho bila kujali dini , kabila wala itikadi zake .

Wanasiasa wanaweza kuamua tu kutunga chochote na baadhi ya jamii zikabaki masikini na zisifanye kazi au kuendelea maisha yao yote , kwa sababu tu ya tofauti za kiitikadi maajabu ni kwamba wote wanaitwa watanzania .

Siku za karibuni kumetokea sakata zima la Buzwagi ,hili suala ni la kitaifa sio la CCM na CHADEMA au CUF na TLP peke yao , kuna wengine hawana vyama na ni watanzania wanataka kutoa maoni yao kuhusu suala hilo .

Na hata hili suala lingine la Dr Slaa kutaja mafisadi wanaomaliza mali za watanzania , angalia majibu ya Mkono alivyotoa utafikiri alikuwa amelala usingizi wa pono akashitushwa tu , naamini mkono alikuwa anajijua kwamba anakula pesa wa wavuja jasho kwa muda mrefu .

Mkono akaamua kuwaingiza watu wengine zaidi katika suala lake akamrukia Marando , na upande mwingine akamrukia Maira wote hawa sasa wameingizwa katika siasa sasa fani ya sheria imegeuzwa kuwa siasa na mradi kwa wengine .

Viongozi wa Vyama vya upinzani waliooanza ziada za mikoani kuwatangazia wananchi mabaya ya CCM kwa wananchi ambao hawana elimu imara kuhusu uraia na mambo mengine ya nchi yao ilionekana kama mchezo wa kuigiza vile .

Nimeshangaa kwa nini hakuna mtu anayehoji hizo pesa za kuzunguka na helicopter wapinzani wamezipata wapi ? kwanini pesa hizi wasingetumia kuzindua mradi mmoja kila wanapotua na helicopter , au basi wawe na elimu maalumu kwa wanachi kuhusu uraia ?

Hivi ndio vitu vya kufanya kabla ya kufikiria mambo mengine yote ambayo yanaweza kuchonganisha wananchi na serikali au serikali na chama cha mapinduzi na mambo mengine kama hayo , tena haya mambo hayahitaji mitaji mikubwa .
Kama nilivyosema hapo juu siasa ni mchezo wa ajabu sana , nacho chama cha mapinduzi kimeamua kuzunguka mikoani kujisafisha , lakini wakumbuke kwamba wanaozunguka ni mawaziri ambao pia ni wabunge , wengine bado wana fani zao serikali .

Hawa mawaziri wanaozunguka na CCM sio wasemaji wa CCM au Serikali na sijui kama matamko yao yanawakilisha Serikali au CCM hakuna anayetaka kujua hilo lakini ni vizuri tukatofautisha Serikali na Siasa .

Kama mtu ameteuliwa kuwa waziri yeye hatakiwi hata kidogo kujihusisha na mambo ya kampeni ya chama chake na hata kwenda mikoani kutangaza sera za chama chake kwa sababu anatumikia serikali ambayo haina dini , chama wala matabaka .

Hata askofu mkuu wa KKKT ameshaonya serikali kuhusu masuala mengi haswa kuhusu mafisadi lakini hawa viongozi wa dini hawafanyi chochote cha zaida , mfano lowassa ni mlutheri alitakiwa akatazwe kuingia kanisani pale Mbezi Beach Tangi Bovu . na kanisa lingine lolote la KKKT

Kama mapuri alivyokuwa anagomewa kuingia msikitini kule pemba , kwa viongozi wengine wanaofanya mambo ya ajabu ajabu tunaweza kuwagomea pia hili halina ubishi na tunaweza kulitekeleza kwa kushirikiana kwa namna moja au nyingine .

Au wakati mwngine tunajua kwamba kikwete anakuja kuhutubia mkutano moshi vijijini basi hatuendi katika mkutano huo hata chembe mpaka ajibu tuhuma zinazomkabili kuwazomea haitoshi , zaidi ni kutokwenda katika mikutano yao na mihadhara yao mengine
 
Kumbukumbu tuu ya huyu member mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki, bandiko lake hili halikuchangiwa na yeyote wali halikupata hata thanks moja, leo ndio nimempa thanks na kumuenzi kwa kuchangia. Mimi ni muumini wa life after life, hivyo marehemu huko aliko, anafurahi sana kusoma tunamkumbuka.
RIP Mkuu Yona Feres Maro, aka Yoyo.
Mode weka alama ya RIP, wageni wengi humu kila uchao.
P
 
Big up P
 
Back
Top Bottom