Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,056
Kamapeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu zimeingia wiki ya tatu huku ikiwa inajulikana sasa ushindani mkubwa upo kwa vyama vya CCM na CHADEMA.
Mwanzo wakati kampeni zinaanza kulikua na kutegeana ili kusikia mwenzako ameongea nini ili umkosoe na kumzodoa ila sasa naona kila mgombea anajipambanua kwa haiba yake mwenyewe na sera ya chama chake.
Kuna hoja iliyopo kwenye sera za CHADEMA, hoja ya kuwa na serikali za Majimbo naona imepamba moto. CHADEMA wanasema huo ndio muarubaini wa kuhakikisha Wananchi wanafaidika na rasilimali zinazopatikana katika maeneo yao na sio kila kitu kupelekwa serikali kuu kisha warudishiwe kidogo kama ruzuku. Mahali ambapo kuna mapungufu kutokana na uchache wa rasilimali serikali kuu ndio itaongeza nguvu.
CCM kupitia Mgombea wao wanapinga na kusema kwamba hiyo ni sera ya kuigawa nchi na kutaleta matabaka ya kiuchumi, kikabila na hata kidini. Ni sera ambayo msingi wake ni wakikoloni. Pia kuna maeneo ambayo hayana rasilimali za kutosha kwahiyo kuna uwezekano yakaachwa nyuma zaidi kimaendeleo na kwamba sera ya mikoa kama ilivyo sasa ndio muafaka wa kuleta maendeleo ya watu.
Bila kujali sera ya chama kipi ndio nzuri nadhani wote wanastahili pongezi kwa kuanza kuleta mijadala ya sera na hoja ili wananchi waweze kupima na kuamua. Kama kuna uwezekano wagombea wajitahidi kupunguza ukali wa maneno/lugha na hakika kampeni za mwaka huu zitakua zenye ubora (quality) kuliko nyingi zilizopita kwa sababu yanaongelewa masuala na hoja nzito.