Hizi nafasi za Nbc na zakweli

mr timber

JF-Expert Member
Feb 7, 2016
263
189
Hi team

Kama una mdogo au ndugu yako hajaajiriwa na anatafuta ajira. NBC Bank wametangaza nafasi za muda mfupi(miezi 5 to 6) so kama yuko tayari tafadhali mwambie kesho asubuhi aende NBC HQ kwa walioko Dsm au kwenye branch za NBC kwa walioko mikoani.

Amuone Branch Manager na ajitambulishe kuwa ameenda kufanya aptitude test kumbuka test inaanza saa 3 asubuhi hivyo awahi asisahau CV yake kiwango cha elimu kinachohitajika ni degree
 
Sidhani kama kuna ukweli hapo.. Ile ni institution kubwa, haiwezi kutangaza ajira kwa style hiyo hata kama ni temporary. Na pia tangazo halina tarehe.. Huwezi kusema "kesho" tu haitoshi. Ni uzushi
 
Hii ishu niliiona whatsapp tarehe 26, leo jioni nikaiona tena, usiku huu nimeikuta hapa naamini ni uzushi.
Kesho ya mwanzo kabisa haijafika tu?
 
kama kunaanaejua ukweli naomba atujuze tafadhali mfano mm nina sababu nyingi tu za kuitilia mashaka lkn kutokana na hali jinsi ilivyo kitaa nibora nikashangae town hyo kesho isiokua na trh maana kuna jamaa yangu kasema yy kaipata toka jana, btw kama kuna mwenye ukweli plz weka mambo adharani ndugu yako niokoe nauli natajiungia bundle hata mwakani
 
My bro kaenda wamesema hawana taarifa hiyo posta branch.. Kawakuta wenzie wa3 so aliyewapokea kachukua Cv tu.... Akawaambia huwa wana agents wa kuwatangazia ajira... Wakaulizwa kama kuna fee yoyote waliotozwa maana wao hawausiki na hawajui.. So ikabid tu waondoke ila CV wamechukua
 
Roho inaniuma sana wasomi wanavodharaulika nchi hii, haya sijui yatakwisha lini? Tatizo la ajira linafanywa wasomi wamekuwa kama mpira wa kona. Sad! sio Tanzania niliyoitarajia wakati nilipozaliwa nchi hii
 
wasomi tunadharirika sana sababu hatutumii akili zetu kutajirika... wengi hatuna mitaji ila hata mawazo yetu pia hafifu hata ukiuliza wasomi wengi anataka afanye nini hana majibu zaidi ya kilimo ambacho hata hajui atalima nini na soko atauzia wap??

elimu ni zaidi ya vyeti
 
Hiyo habari ni ya ukweli, mimi nilitumiwa taarifa whatsap jana asubuhi saa mbili naingia whatsap nikaiona nikajianda faster nikawahi nilivyofika pale reception nikawaeleza nikaandika jina kwenye kitabu cha visitor..baada ya muda mchache tuliambia tuende floor ya 7 nilivyoingia tukakuta watu wengi tu ambao walikuwa tayari wao walishafanya na sisi tukaingia chumba cha mtihani tukafanya maswali yalikuwa 20 kila moja marks 5, hili ufanikiwe kuitwa kwenye oral unatakiwa upate 50% majibu walitoa jana hile hile hila mimi nilipata 45%. Ivyo sikufanikiwa kuendelea na oral. Hiyo inshu ni serious hila ilikuwa ni jana tarehe 29/12/2016 ndio interview ilifanyika.
 
Sio hila ni ila...
 
Poleni mchumia juani kwa kweli
46738a70732cff4f0cf9460077615ad6.jpg

Mungu amlaani huko aliko
 
Back
Top Bottom