Hizi Mbinu, Polisi walijifunzia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi Mbinu, Polisi walijifunzia wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Andindile, May 10, 2009.

 1. Andindile

  Andindile JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Polisi wamweka rumande mtoto babake ajitokeze Sunday, 10 May 2009 09:58 Na Glory Mhiliwa, Arusha

  JESHI la polisi Mkoa wa Arusha linamshikilia mtoto wa miaka tisa aitwaye Richard Grayson mkazi wa Shangarai ili kumshinikiza baba yake anayetuhumiwa kuhusika katika matukio ya ujambazi ambaye anadaiwa kukimbia kusikojulikana kujisalimisha.

  Tukio hilo lilitokea juzi alfajiri majira ya saa kumi na moja baada ya askari polisi wakiwa na gari aina ya Land Rover Defender kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambapo walipomkosa waliamua kuondoka na mtoto huyo.

  Mtuhumiwa huyo Grayson Mollel (34),Jeshi hilo linadai kuwa linamtafuta kutokana na tuhuma za ujambazi zinazomkabili. Hata hivyo halikuwa tayari kutaja baadhi ya matukio ya ujambazi ambayo mtuhumiwa huyo anadaiwa kuhusika nayo.

  Akizungumza na Majira Jumapili kuhusiana na tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Bw. Basilio Matei alisema kuwa taarifa za mtoto huyo kushikiliwa ili kumshinikiza baba yake kujisalimisha hazijawasilishwa kwake.

  ‘Mimi ndio kwanza nasikia kutoka kwenu lakini naahidi kufuatilia ili kujua ukweli wa tukio hilo kama kweli mtoto huyo alikamatwa na kulazwa rumande kwa kosa ambalo linamhusu baba yake nitawapatieni taarifa kamili’ alisema Basilio.

  Aidha mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu shule ya msingi ya Moivo wilaya ya Arumeru anadaiwa kutiwa nguvuni na askari polisi wakiwa na silaha baada ya kuvamia nyumbani kwao eneo la Shangarai wilaya ya Arumeru.

  Hata hivyo askari hao baada ya kumchukua mtoto huyo walimwamuru wamweleze baba yake alipo ambapo aliwaelekeza nyumba ya mama yake mdogo ambae ni mke mdogo wa baba yake anayeishi Sanawari. Hata hivyo hawakufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na ndipo walipoamua kumkamata na mama huyo pia. Aidha mama huyo aliyefahamika kwa majina ya Georgina Grayson alikamatwa na kuswekwa rumande kama ilivyo kwa mwanae

  Hatua ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka tisa aliyekuwa ametoka hospitali ya wilaya ya West Meru alipokuwa akiuguza kifua baada ya kuanguka kwenye mti kumetafsiriwa na wananchi kuwa jeshi la polisi linakiuka haki za mtoto. Bi Neema Florence ambae ni mkazi wa Shangarai anasema kuwa mtoto huyo ni mdogo sana
  kulazwa mahabusu ya watu wazima tena kwa kosa alilofanya baba yake.

  Mtoto kakosa nini?
   
 2. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Jeshi la polisi halina mamlaka ya kumzuia mtoto huyo. Hakuna sheria inayosema hivyo, pili kama wanamtuhumu mtoto huyo basi walitakiwa wamfungulie mashtaka. What a crap!
   
 3. Yombayomba

  Yombayomba JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Aug 23, 2006
  Messages: 818
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii imenisikitisha saana kwani ni ukiukwaji wa haki za binadamu, labda kama mtoto pia anashiriki au wanahisi kafundishwa. Lakini kama bado basi tayari wamemuharibu mtoto kwa kuanza kumfundisha na sitashangaa kama hawajamfinya kengere zake
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  This is a tort of false imprisonment and the young boy deserves to be compensated, he should be encouraged to go to Court and claim. In that way the police force will start working according to principles and not threats and intimidation.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mbaya zaidi ni wa miaka 9! What an inhumane hehavior?

  Tunategemea wanasheria na wapenda haki za binadamu watalivalia njuga

  suala hili na kuhakikisha kwamba mtoto huyo anaachiliwa mara moja na

  kwenda shule.

  Huko rumande anaishiishi vipi! Kwa umri huo anafundishwa tabia mbaya na

  chafu sana bila sababu yoyote. Je jeshi letu limeishiwa mbinu za kumsaka

  mhalifu kabisa na kufikia kugundua sayansi mpya hii ya utafutaji

  watuhumiwa?
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hii ni kidnapping, literally speaking.
   
Loading...