Hizi huduma za nssf vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi huduma za nssf vipi?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Escobar, Apr 16, 2012.

 1. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Mdogo wangu amekuwa akifuatilia madai yake tangu mwanzoni mwa mwezi wa pili pale NSSF Ilala. Alipojaza fomu aliambiwa arudi baada ya wiki mbili tu kila kitu kitakuwa tayari! Hivi ninavyoandika hapa ni mwezi wa pili kilasiku anapigwa kalenda na kinadada wa pale mapokezi, kila akifika pale ni ama bosi hayupo na hajasign cheque au mtandao uko chini. Naomba waandishi wa habari watembelee pale japo kwa mahojiano na wateja wowote mtakao wakuta ili mjue usumbufu na manyanyaso wayoyapata watanzania hawa wa hali ya chini baada ya kupoteza kazi kwa zaidi ya miezi sita na maisha yenyewe haya ya Dar es Salaam. Kutokana na usumbufu alioupata ndugu yangu mimi binafsi na workmate wenzangu tumeamua kuconvert to PPF japo siijui vizuri sana ila tu sitaki kusikia kitu kinaitwa NSSF tena maana mimi mwenyewe nimeshamsindikiza pale 3 times anaenda kuambulia story utadhani kaenda kuomba mkopo au msaada. Mbaya zaidi nasikia mkurugenzi wake yuko busy na harakati za kutaka ubunge huko kwao mafia huku shirika linadoda kwa utendaji mbovu!
   
 2. Ikumbilo

  Ikumbilo JF-Expert Member

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 455
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  NSSF ni janga la kitaifa. Sio tu Dar hata sehmu zingine ni hivyo hivyo. Sasa sijui jamaa wanafurahia kuona watu wanakwenda kila siku ofisini kwao ili waonekane wanahudumia?

  Pia unajua Customer care yao ni mbovu tena haina hata kumbukumbu. Utaambiwa njoo baada ya wiki mbili ok, ukirudi hizo wiki mbili unaambiwa kalikwenda kalirudi. Je hizo wiki mbili mlizoniambia nije zilikuwa na maana gani? Je kuna mtu anayetunza kumbukumbu za hao wateja wao hadi anamwambia aje baada ya wiki mbili? Au huwa wanatamka kukuondoa usikate tamaa?

  Kuna mengi sana ya kuandika lakini mikono inasita, ila kwa mie ambaye ni miongoni wa waathrika wa NSSF nasema NSSF ni janga la kitaifa.
   
 3. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Mkuu unaweza kunipa msaada jinsi ya kufanya the needful hapo kwenye red. NSSF is behind PPF for Everything. kama PPF unapata mafao yako Ndani ya siku tisini iweje hawa NSSF washindwe.? Eti mpaka baada ya miezi 6 ndio u Claim. huu ni unyanyasaji Live live. halafu baaada ya miezi sita bado m2 anasumbuliwa.

  Nafikiri hili suala tuliongeze pale kwenye uzi wa marhemu Regia Mtema kuhusu Kero zetu tunazohitaji zizungumziwe Bungeni.
   
 4. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Kuna mdau alituambia kuwa PPF huduma zao kwa sasa ni angalau nafuu maana unapata kilicho chako ndani ya wiki tatu hadi nne hivyo nikaona ni bora wao kuliko hawa jamaa wa NSSF maana tayari nimejionea mapungufu yao, kuna kinadada pale NSSF ILALA wanamajibu ambayo yalinitia shaka ueledi wa kazi zao, sijui ndio watoto wa wajomba na shangazi, i wish wangekuwa wanapewa training za customer care maana hawajui kuwa mtu anayekuja pale tayari anamatatizo kibao nyuma yake ila wao wanakutreat kama umepotea njia na wala hukupaswa kuwa pale! Kuna mdau alisema Mr. Crescentius Magoli yuko NSSF na ninavyomjua ni mpambanaji na asingependa kuona huu ujinga, tulijaribu hata kutafuta namba yake but hatukufanikiwa maana walioko juu sometime huwa hawajui uozo ulioko chini hasa kama wanotendewa hawasemi na kuendelea kuumia kimoyo moyo!
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,924
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280

  hivi inawezekana kuhamisha michango kutoka NSSF kwenda PPF?
   
 6. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Nadhani kuhamisha haiwezekani ila mimi nimeamua kusitisha michango yangu kwenda kule kuanzia mwezi huu na baada ya miezi sita lazima wanipe changu! Kama ni barua ya kujifukuza kazi nitawapelekea maana wamemtesa sana yule bwanamdogo so sina hamu nao hata chembe! Lakini wakati wanakuja kutushawishi tujiunge nao miaka 5 iliyopita walikuwa wapole na wataratibu kuliko kawaida, tukawa tunaahidiwa hata kuuziwa nyumba mpaka leo sina ninayemjua mimi aliyewahi kanunua nyumba NSSF!
   
 7. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  PPF ndani ya mwezi unachukua chako.Ukiwa na sababu genuine hata ndani ya wiki unapata. Hata kama wana mapungufu mengine lakini kwa hilo nawapa credit. Chukulia kibarua kimeota nyasi na mtu hana akiba yoyote anategemea mchango wake angalau apate nauli ya kurudi kwao then unamzungusha miezi!
   
Loading...