Hivyo haya matatizo ya wanafunzi serikali haiyaoni kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivyo haya matatizo ya wanafunzi serikali haiyaoni kweli?

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Mar 18, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Wanafunzi wa darasa la Nne wa Shule ya Msingi Muhogwe iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Uyui mkoani Tabora wakiwa na mwalimu wao akifundisha huku wanafunzi hao wakiwa wanaandika wakiwa wamekaa chini. Shule hiyo inaupungufu wa madawati 70.


  [​IMG]

  HAYA NI KWELI MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA HONGERA CCM
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,787
  Likes Received: 36,794
  Trophy Points: 280
  Kuichagua CCM ni kuchagua maisha magumu kwa kila mtanzania.
  Kuitetea CCM inahitaji uwe na akili ya maiti. :frusty:
   
 4. Pindima

  Pindima JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2012
  Joined: Aug 16, 2011
  Messages: 349
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tuchague chama gani?!!
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  chagua chama chenye kuleta maendeleo hapo kwetu Tanzania........................... Utajaza mwenyewe ni chama gani??????????????????????????????????????
   
 6. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #6
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nasikitika sana ninapoona vijana wenye akili timamu wanaamini katika ndoto za 'Maisha Bora kwa kila mtanzania ndani ya CCM iliyopewa 50 yrs ikashindwa". Hakika wana disorder(s) katika ubongo wao!
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Ndio itabidi tuamke kuwachaguwa viongozi bora ili nchi yetu iendelee kimaisha na kiuchumi Tusibabaike na majina ya vyama tu Tuwaangalie Viongozi bora wanaopenda Maendeleo ya nchi na Wananchi wake.
   
 8. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
   
 10. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  usijali mkuu watapatiwa madawati uchaguzi ukifika
   
 11. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #11
  Mar 19, 2012
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Inatakiwa njia nyingine ya kupata viongozi, tumeshuhudia matokeo yanayo tangazwa hayana ukweli na hali halisi. Haiwezekani nchi ikawa na wajinga wasio ujua ukweli. Mfano jamaa kaweka ahadi za jamaa anayejiita Rais, wakati alijiingiza mwenyewe hata hatujui alipata kula ngapi.[​IMG]
  AHADI: Tunayomdai Mshindi

  Ahadi za Kikwete:


  • Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
  • Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  • Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  • Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  • Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  • Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  • Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  • Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  • Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  • Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  • Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  • Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  • Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  • Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  • Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  • Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  • Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  • Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  • Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  • Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  • Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  • Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  • Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  • Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  • Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  • Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  • Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  • Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  • Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  • Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  • Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  • Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  • Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  • Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  • Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  • Kulinda haki za walemavu- Makete
  • Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  • Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  • Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  • Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  • Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  • Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  • Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  • Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  • Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  • Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  • Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  • Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  • Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  • Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  • Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  • Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  • Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  • Kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  • Kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  • Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  • Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kibandamaiti mjini Zanzibar
  • Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  • Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  • Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  • Kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  • Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  • Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  • Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  • Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  • Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  • Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
  Hajawahi fanya hata kitu kimoja!!!!!!!! Nenda kwenye kampaini zao usikie ahadi za uongo!
   
 12. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  Na bado mkoa unaongoza kwa kuwa na mapori mengi yenye wanyamapori
  bado madini yapo
  Bado kilimo cha tumbaku

  Ila shule zake ndo hizo wanafunzi wanainama kwenye kuandika
  na kesho uchaguzi ukija watakichagua chama chao kile kile na ahadi zitakuwa zile zile
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Haya yote uliyoyasema ilikuwa Mkuu Rais wakati wa kampeni yake ndio aliyotoa ahadi kuwa atayatimiza? Kama ndio hivyo ilikuwa ni moja ya Kampeni zake ili umpe

  kura zako ili apate kuwa Rais wa nchi hatoyatimza hata kidogo Mpaka atakapomaliza URais wake hayata timia kamwe. Nijuavyo mimi neno Siasa maana yake ni Uongo wa hali ya juukuwafanya Watu wengine wawe wajinga kuwadanganya kamaneno mazuri , kwa

  mfano moja ya hao Viongozi wanaotaka kuchuguliwa husema hivyo natoa mfano mimi Mkinichaguwa nitawaleteeni mabasi ya gorofa mimi mukini chaguwa nitawajeengeni mabarabara yanayopita juu ya nyumba hizo tu mojawapo ni njia ya kampeni ya kupata kura za

  Walala hoi ili apate kushinda katika Uchaguzi kuwa ni Kiongozi hakuna hata kitu kimoja kitakacho fanyika hapo ni uongo mtupu Mkuu mambo ya Siasa.
   
 14. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Katika ahadi zote iliyoniacha hoi ni ya "KUZUIA HATARI YA KISIWA CHA PANGANI KUZAMA - TANGA" Na bado wapenda khanga, t-shirt na kofia za kijani bila kutafakari wakapiga makofi na kumchagua!
   
 15. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Hapo ndipo palipo na tatizo kubwa la watanzania Ndugu yangu Mr Rocky? Katika makala yangu ya "salamu zangu zikufikie..mjomba daktari" Niliuliza Maswali mengi yakiwemo je ni viuno vya wasanii wanaocheza jukwaani wakati wa kampeni vinavyowachanganya wananchi? Je ni Pombe wanazopewa wakati wa kampeni zinazoharibu akili zao?
   
Loading...