Hivii kuoa/kuolewa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivii kuoa/kuolewa...

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jun 7, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  .... ndo mwisho wa kua na marafiki wa jinsia tofauti???

  Nauliza kwasababu naona watu hua wanalaani sana msichana mwenye “rafiki“ mwanaume aliyeoa au msichana aliyeolewa akiwa na “rafiki“ mwanaume.
  Upande wa wanaume sijasikia malalamiko sana na nnadhani hii inatokana na zile fikra kuhusiana na “wanawake kua wepesi sana kushawishika pia kishawishi na bila kusahau wanawake kuwa wadhaifu.“

  Naomba kusema kwamba binafsi sioni tatizo iwapo heshima stahili ipo kwa pande zote na kila mmoja anajua mipaka ya urafiki wao.Mimi nimewahi kua na rafiki aliyeoa na hatukua na matatizo yoyote.Japo sikupata bahati ya kukutana na mke wake ila tulitambulishwa na kujuliana hali mara kadhaa.
  Nwy nachojaribu kuonyesha ni kwamba kama kuna urafiki wa kweli bila kua zaidi ya urafiki sioni tatizo la watu wa jinsia tofauti wenye wenza wao kua na marafiki wa jinsia tofauti!!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Ukija olewa jaribu kuwa rafiki yangu uone
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndo mchango wako huu?!

  Enhe itakuaje kwani?!
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Ndo mchango wangu ndiyo. Kwa nini unashangaa? Kushangaa hakuruhusiwi hapa. Kama unataka kushangaa kashangae feri huko ambako shilingi inazama na meli inaelea. Ebo!
   
 5. CPU

  CPU JF Gold Member

  #5
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lizzy
  Niki-refer ulivyosema wewe ni mwanamke lakin una hisia za kiume naweza kuamini kuwa unaweza kusimamia ulichosema (65%)
  Fahamu kwamba kila binadamu ni dhaifu, na udhaifu hauna mipaka.
  Kutokana na huo udhaifu, binadamu anaweza kubadilika wakati wowote (throu ushawishi and so)
  Nadhani umewahi kusikia mtu akisema " Wakati tunaanza kufahamiana ilikuwa kawaida tu, wala sikuwa na hisia zozote kwake. Ulikuwa urafiki wa kawaida tu, hata mke wake alijua.
  Lakin nikajikuta naanza kumpenda, yaani hata sielewi imekuwaje. Najua ni mume wa mtu lakin nimeshindwa kujizuia, ananijali, ananiheshimu, ananipenda, ananisaidia . . . . najisikia kumpenda"

  Wimbo wa wadada wawili waitwao Dataz unaosema Mume wa mtu umeongea mambo haya.
  So urafiki unawezekanika lakin udhaifu hauzuiliki na wala haujali status ya mtu

  Conclusion
  Kujenga mazoea sana na mwanandoa wa mtu ni vyema lakin inaweza kuzaa usaliti
   
 6. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,034
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Lizzy! Ukiolewa, marafiki wanapukutika wenyewe!
   
 7. CPU

  CPU JF Gold Member

  #7
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Swali lako lime-generalize watu wote bila kujali status zao
  Ungeuliza "ndio mwisho wa kuwa na marafiki waume au wake za watu???"

  Na kwanini ujizoeze kwa mwanandoa wa mtu??
  Marafiki wema wameisha?
   
 8. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #8
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Mimi nina mtazamo tofa na uti! Wazo la kujenga mazoea ama urafiki na mwanandoa wa mtu siafikiani nalo kihivyo hususan ukiwa ule urafiki wa jinsia tofa na uti. Amini usiamini mara nyingi hiyo huwaga chanzo cha migogoro mingi sana katika ndoa.

  Hebu piga picha bwana CPU. Eti Ngabu na my waifu wako ni washikaji. Aahahahahahaa….daaah ebana eeh utaweza kweli ku-handle hiyo kitu? Utakuwa na amani kweli? Eniwei sijui, ila watu tumetofautiana sana na huenda labda wewe ikawa si ishu kwako. Lakini mara nyingi sana marafiki wa jinsia tofa na uti huwaga ni moja ya vyanzo vya migogoro kwa wanandoa. Binafsi sishauri hivyo. Ni mtazamo tu.
   
 9. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #9
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Swali limeanzia kwenye kichwa cha habari...unganisha!!

  Khaaaa ina maana mtu aliyeoa/olewa sio/hawezi kua rafiki mwema???Aisee hii ni mpya kwangu!!
   
 10. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Dah....ngoja nibaki kua muangaliaji basi!!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haya nimekuelewa gubbe....
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Hilo kama ni tusi basi mwenyewe mara mia nane hamsini na tano!!
   
 13. CPU

  CPU JF Gold Member

  #13
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ngabu
  Kama nikioa
  Kwa mimi CPU siwezi kwa kweli, nakiri wazi kabisaaaaa.
  Hata waifu anihakikishie vipi kuwa hatatoa bado sitakuwa na amani
  Likitokea tatizo dogo tu naweza kuanza kuhisi tatizo ni uhusiano wake na Ngabu (on first attempt)
  Ila yeye Lizzy anajifanya ataliweza, labda apate mume ambaye hajampenda (yaani wivu is equal to zero)
  Otherwise atakuwa anasababisha migogoro na mume wake bila kujijua, halafu akaona mumewe ana matatizo.
  Then aanze kuja kupost ma-thread ya kuomba ushauri
  :becky::becky:
   
 14. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hahahahhahahha
  Owkey kille basi.....sifa hizo nakupa ujue!:majani7:
   
 15. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #15
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Wow!! Super big ups my dude. That's what I call too much truth.

  Yaani umekuwa mkweli na muwazi bila kumung'unya maneno. Mad respect.
   
 16. CPU

  CPU JF Gold Member

  #16
  Jun 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Tatizo sio urafiki mwema, tatizo uhusiano na mume wa mtu unajenga picha mbaya kwa jamii na hata kwa mke wa mwanaume.
  Wewe ulie nje ya ndoa unaweza ukaona poa tu, lakin wenzako wakikwaruzana kwenye ndoa yao wanaanza kukutajataja kama chanzo
  Unaona ni mazuri hayo???
   
 17. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #17
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Sifa gani hizo unazonipa? Hilo neno "gubbe" limekaa kama tusi tusi flani hivi. Na sijui umeliokota wapi. Tafuta neno jingine bana…."gubbe" silitaki mimi.
   
 18. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee...sasa huo ndo ule wivu unaozidi mpaka kero.Yani mtu wa aina hiyo hata Sipiyu akinigongea Thanks na Like JF ananiuliza kwanini fulani kakugongea thanks?Embu kuweni na imani bwana....hata asipokua nao bado anaweza asiwe muaminifu vile vile.Kuwa mdanganyifu ni hulka ya mtu na sio swala la yeye kua na marafiki wa jinsia tofauti au la!!
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  We nawe acha kudeka ...sinimeshabadilisha??Sasa hivi ni KILLE!!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jun 7, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Sawa, udanganyifu ni hulka ya mtu. Hilo mimi sikatai. Lakini kubali usikubali urafiki wa jinsia tofauti na mwanandoa ipo siku utaleta mzozo ndani ya ndoa.

  [FONT=&quot]Na haya mambo ya imani pofu mimi sikubaliani nayo. Cha muhimu ni wewe uliye kwenye ndoa kutokumpa mwenzako hata chembe ya sababu kukudhania kuwa unafanya mambo ambayo hutakiwi kufanya. Na kama kweli hufanyi jambo lolote baya basi na mwenzako naye wala hatakuwa na sababu ya kukushuku.[/FONT]
   
Loading...