Hivi Wazungu masikini nao wakitajirika ghafla huanza dharau kama baadhi ya Waafrika waliozibahatisha?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,023
Yaani Mswahili (Mtanzania) akiwa na maisha ya kimasikini/kifukara kama GENTAMYCINE siku akizibahatisha/akizipata tu ghafla utamuona anaanza kubadilika kitabia kwa kuanza kuwa na maringo (majipu), dharau, sanifu na unafki mwingi.

Sijawahi kwenda au kuishi Ulaya (Marekani) na sitarajii kwenda huko kwani ugali wangu wa Kizanaki na Kimakuwa na mboga zetu zinanipa raha na amani ya kuishi Afrika (Tanzania) ila naomba kujua kwa nyote mlioko huko je, na hawa Wazungu nao upuuzi huu wanao?

Namuomba sana na mno Mwenyezi Mungu siku tu akija kunibariki na utajiri wa kutukuka GENTAMYCINE nisibadilike kitabia, tena ikiwezekana niwe mtu wa Imani (dini) kabisa na 75% ya utajiri wangu niutumie kusaidia ndugu zangu wenye shida, watoto yatima, wajane, wazee na wagonjwa wasiojiweza wanaotaabika hospitalini.

Happy Union Day Watanzania wote.
 
Back
Top Bottom