Hivi watanzania tumelaaniwa au????

Babu Lao

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
2,043
179
Leo nilikuwa natafuta mbuga za wanyama za nyumbani.. nimeshangaa sana kuona kuwa ni mbuga moja tu iko online, Saadani National Park ndio pekeee unayoweza kuipata online.. Cha ajabu the might serengeti-tz haipo wakati masai mara-kenya ipo, hivi kweli tupo serious watanzania???? Na nimeona mbuga ya mkomazi national park wanaitangaza iko kenya (http://www.youtube.com/watch?v=FSzeKVgv6tU), hivi ni lini tutaamka sisi watanzania kila siku tunalaumu watalii wanaanzia kenya.... kama watu walopewa mamlaka ya kusimamia rasilimali zetu hawako makini kiasi hiki????:A S 13::A S 13:
 
Pole sana Mkuu. Mimi mwaka fulani nilikuwa kwenye Embassy ya Kenya, nchi kapuni, Jamaa walikuwa na picha ya Mlima wa Kilimanjaro ambao upo kenya. Nilipo wauliza kulikoni Mlima huu kuwepo kenya, jamaa wa embassy yao akadai ni kutukuza mali zetu za afrika mashariki. Kumbuka, hapo, nilikuwa na kajamaa ketu ka embasi na kalikuwa kimyaa kama maji ya mtunguni.


Tusubiri labda na sie wadanganyika tutakuwa na 18 bora kama Misri. Au mkoloni aje na arudishe mijeredi ndio akili zitaamka.
 
Haya mambo yanatia hasira sana, Yaani mtu akishapewa mshahara na akiiba alichoiba ndo basi tena hata HAKUMBUKI KUUMA NA KUPULIZA!
 
..ngorongorocrater.org ipo sijui kama uliiona hii, ninayo pia docu yao waliyotengeneza

..pia serengeti.org ipo soooo good (imetengenezwa kitaalamu kweli, inavutia na iko interactive) hebu watembelee

..zile zinazotoa habari za ujumla ni tanzaniaparks.com na tanzaniatouristboard.com

..tatizo la uendeshaji wa nat parks, game reserves and the like in TZ ni kwamba sio zote zenye mandate yao wenyewe (mf. Ngorongoro), nyini zinazobaki zipo chini ya TANAPA and therefore TANAPA anakuwa responsible kuzitangaza na si kila moja peke yake. Tofauti na uendeshaji wa parks huko Kenya au S. Africa kwa mfano.

..huku kwetu parks haziwezi ku-compete against each other, because the whole thing goes to the same coffers (TANAPA), ambao ingawa hawafanyi kazi nzuri sana lakini tukizingatia na background ya hii industry you can't put much blame.

ni mtazamo tu
 
Back
Top Bottom