Hivi wanawake nyinyi mna nini?

Adharusi

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2012
Posts
14,506
Reaction score
7,445
Nimejiuliza sana kwanini miji mingi Tanzania ukikuta nyumba mmiliki ni mama basi imelithiwa kutoka kwa marehemu mumewe,sijabahatika kukuta nyumba imelithiwa na Baba,inamaana wanawake awajengi ili na sisi tulithi au mali ya baba ni ya wote na yamama yake peke yake
Naomba majibu
CC madame B,FF,ASHaDii,rala 1,mamndenyi
"Vox popoli vox dei"
 
mali za ndoa ni za wote wawili, labda kwa kukuongezea hii inaonesha wanaume wanawahi kufa kuliko wake zao ndio maana wanawake wajane ni wengi zaidi na hivyo kurithi mali kuliko wanaume.
 
hee hujui wanaume ni sawa na barafu ilioko Juan?wanakufa hovyo hawa kama kuku wa kizungu wee waone tu na dushelele zao ambazo cku hizi zimeathiriwa na chips mayai basi akipiga kimoja tu na povu likatoka anajua kapiz lazma wanawake warithi kwa sababu mwanamke hafi hovyo na pia mwanamke ni mtu makini siku zote
 
Tena kwa wanawake wa kirangi,baba ukioa na kujenga kifo hakipo mbali take care.

wamachame, nao mchezo ndo huo, wengine ni wajita - kama huamini nenda msoma kuna mtaa mmoja wenye nyumba ni wanawake tu.

Hapa town kuna mama mmachame alishawaua wanaume 2; sasa anamiliki zile kampuni na majumba walojenga hao wababa.
 
una uhakika????? mbona hukumreport police???? acha uzushi.....
 
wamachame, nao mchezo ndo huo, wengine ni wajita - kama huamini nenda msoma kuna mtaa mmoja wenye nyumba ni wanawake tu.

Hapa town kuna mama mmachame alishawaua wanaume 2; sasa anamiliki zile kampuni na majumba walojenga hao wababa.

Je hakuna vifo vya kawaida
"Vox popoli vox dei"
 
Duh! Umeamua kujibu mashambulizi! Maana wiki hii ukizama kwa thread tuu.. PTAA! za usoni kwenu (w/ke)!
Haya na wewe chukua zako hizi:- nyinyi wenyewe ndio mnaupeleka mbele mfumo dume kwa uvivu wa kutojenga hata kama mnauwezo! Mnasubiri m/me kafanikiwa, mnamuua then mnajirithia! Afu mnasingizia tunakufa hovyo! Mbona waume maskini hawafi hovyo?
 
..........Kuhusu nyumba miaka hii hata wamama wanazo nyumba walizojenga wenyewe,
wanaume wanaona aibu kuridhi nyumba za wake zao ujue.
 
Nenda mbeya kule nonde au mabatini
na sasa sae nyumba zote wamebaki wanawake,
sijui ni mipango ya Mungu au ni mikono yao
napata tabu kujua hili; saidia hapa.

wamachame, nao mchezo ndo huo, wengine ni wajita - kama huamini nenda msoma kuna mtaa mmoja wenye nyumba ni wanawake tu.

Hapa town kuna mama mmachame alishawaua wanaume 2; sasa anamiliki zile kampuni na majumba walojenga hao wababa.
 
wanaume wengi wanaoa wanawake wadogo ki-umri, 10yrs younger than them, hivyo ni kawaida kufa kabla ya mke. Pia stress za kutafuta pesa zinachangia kukuua haraka. n.k.
 
Khaaa maswali mengine? Sheria ya ndoa inaweza kujibu hoja ya kwnn wanawake ndio wanaorithi mali za waume zao, na pengine kwa nn siyo wanaume kurithi mali za wake endapo mke ndie alietangulia kufariki.
Wajuzi wa sheria wataweza kutusaidia pengine
 
Kuna maswali mengine ni magumu...
 
mali za ndoa ni za wote wawili, labda kwa kukuongezea hii inaonesha wanaume wanawahi kufa kuliko wake zao ndio maana wanawake wajane ni wengi zaidi na hivyo kurithi mali kuliko wanaume.
Nini sababu ya kisayansi kwa hili.
 
..........Kuhusu nyumba miaka hii hata wamama wanazo nyumba walizojenga wenyewe,
wanaume wanaona aibu kuridhi nyumba za wake zao ujue.

Najua mnajenga siku hizi,haibu tena wakati sina kitu au ndomana ndoa ni ajira kwa wanawake
"Vox popoli vox dei"
 
Ila hapo inaweza kuwa ni kweli
........dada yangu alijenga pale m town miaka ya 80s
hadi leo hii mume wake hajui; siri ya mama na watoto.

Hata hivyo wapo wanojenga kwa wazi tu
japo wanaume mnazikataa pia.

Nyingi zinajengwa kwa kificho kiasi kwamba wanaume wengi wanashindwa kuzijua.
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…