Hivi wanawake mna matatizo gani? (kwa wanawake tu).

Rais Zuma, miaka 70, ametangazwa kuoa mke wa 4. Hii ni ndoa ya 6 kwa Zuma, mke mmoja alifariki kwa kujinyonga na mwingine walitengana, hivyo Zuma atakuwa na wake 4 baada ya kuongeza huyu wa sasa ambaye kwa umri ni mdogo au sawa na watoto wa Zuma.
Nawauliza enyi wanawake, hivi mna matatizo gani? Binti hujafika miaka 40 unaenda kuolewa na mzee ambaye anamaliza maisha yake kesho, ni akili gani?
Wanawake, mna matatizo gani? Ni kutafuta umaarufu? Mnatafuta maisha rahisi (ready made)?
watu wanaangalia mkwanja sio umri
 
na men pia muna problem gan kwann na nyinyi mushaona muna mke mmoja then ukaenda tena kutafuta mwengine s utulie tu ,wake kwa kiume hayo matatizo

Wanaume wanaweza kuwa wanawadanganya na mwanamke akaingia bila kujua. Lakini inakuwaje mwanamke unajua kabisa pale kuna wanawake wengine wawili wameolewa na wewe unakubali kabisa!
 
Mkuu, unadhani unavyofikiri wewe ndivyo binadamu mwenzako anavyofikiri. Pole!

Ah, ndugu, mambo mengine haihitaji akili nyingi, akili ndogo tu inatosha. Binti atakuwa amewapiga chini vijana wa maana anaamua kukimbilia ujane. Labda akisha kuwa mjane atawatafuta aliowatosa.
 
Tatizo letu ni kupenda vionjo vipya hata kama vimetumiwa na wengine. Maadamu hujakitumia basi ni kipya kwangu.
 
Back
Top Bottom