Kwanini Wanawake wanapenda Mteremko?

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Siku za hivi karibuni nilikuwa naongea na dada yangu mmoja anasema anajuta sana kwa sababu mpenzi wake wa zamani amepata ajira ya ualimu shule za serikali.

Dada anasema alifikiria kuwa kwanini aliachana nae pengine angepata hata bahati ya kuwa mke wa mwalimu.

Licha ya dada huyo nae kuwa mhitimu wa shahada ya chuo kikuu tena taaluma ileile ya ualimu bado anatamani angekuwa na Uhusiano na mwanaume aliyepata ajira kwa kuona kama fursa.

Nilishangaa sana kwa mawazo yake nikabaki na Maswali kadhaa ya kujiuliza.

Swali la kwanza nikajiuliza ina maana huyu dada alipoachana na huyo mpenzi wake chanzo ilikua umaskini?

Maana Kama aliachana nae kwa sababu nyingine mbali na umasikini kwanini amtamani wakati alipopata ajira? Sikupata majibu.

Pili nilijiuliza tena je kipaumbele cha Uhusiano wao lilikuwa ni nini upendo au pesa? napo sikupata jibu.

Leo nimekumbuka malalamoko ya vijana wengi wa kiume kuwa wanawake wa siku hizi wanapenda wanaume wenye magari.
Wanasema ukikutana nae atakuuliza "una gari?" Ukijibu hapana atakuuliza tena Unafanya kazi gani? baada ya hapo atasema sawa Kisha ataondoka zake hatopata tena muda wa kujibu SMS wala kupokea simu yako.

Kizazi cha wanawake wapenda ufahari ambao hata hauendani na mwonekano wao.

Kuna mwandishi mmoja aliwahi kuandika "wanawake wenye maumbo mpalanganyiko wanavyopenda kujishtukia" katika maandishi yake alieleza namna ambavyo wanawake hao ni wasumbufu katika mahusiano.

Sasa usumbufu wa wanawake kutaka Wanaume matajiri ndio umetawala kila kona.
Hawajiulizi hata ni nani alijitolea jasho ili mwanaume huyo afanikiwe Ila wao wanawaza tu kuchuma utajiri.

Kuna usemi kuwa kwenye kila mafanikio ya Mwanaume nyuma Kuna mwanamke. Wamesahau hilo wao kutwa kutafuta waliofanikiwa hawataki kuwa nyuma ya Mwanaume ili afanikiwe.

Vijana wanalalamika kuwa mahusiano kabla ya ndoa yamegeuka biashara mwanamke hawezi kukubali pasipo kujua kiasi cha mtaji ulionao "utajiri".

Pia inaonyesha kuwa wanawake wengi wenye tabia hii hawako sawa kisaikolojia, ni limbukeni na hawajajipambanua katika kupambana kimaisha wengi wao ni wavivu.
Hata Wanaume wenye akili wamethubutu kukwepa huo mtego wa wanawake wa namna hii kwa kuweka msimamo thabiti wa kutafuta wanawake wanaojitambua huku wanawake wapenda magari na utajiri wakikosa vyote si mume si pesa.

Peter Mwaihola
 
Wanaume ndio tuna majukumu ya kuoa na dhumuni la kuoa ni kuilinda familia yako kwa hali na mali

Unapoanza familia au kuoa unawajibu wa kuwalisha na kuwahudumia kwa kila kitu
Mwanaume ndio mtafutaji lakini siku hizi unaona wanaume wanakimbia majukumu yao ya kulea

Sasa sijui ni kwanini maana kwa jinsi nilivyokuwa nakumbuka wazazi wa kiume Akina baba ndio wanaohangaika na kuhakikisha mke na watoto wanapata mahitaji yao ya kila siku, haijalishi kama baba anasukuma mkokoteni au ana biashara wote wanahangaikia familia zao

Nimeona Dorothy Gwajima na viongozi wa dini zote wakiongelea haya

Wanawake waliochangia wamesema wanaume hawajitumi inabidi wao ndio wakakope au kufanya biashara ndogondogo ili kuwalisha na baba akiona hivyo ndio anaona mteremko na kutokuchangia chochote nyumbani


Hebu mlijadili hili kwa upana zaidi kwa nini haya yanatokea siku hizi kwa vijana wengi?
 
Back
Top Bottom