Hivi Walimu Wanabeep au Watafanya Kweli?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi Walimu Wanabeep au Watafanya Kweli??

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mr. Zero, Jan 5, 2012.

 1. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,742
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Madeni yasipolipwa shule hazifunguliwi asema Mkoba
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]Send to a friend
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 04 January 2012 20:53
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg

  Gedius Rwiza
  MVUTANO kati ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Serikali ,kuhusu malipo ya madeni ya walimu, unaonekana kushika kasi baada ya Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, kupinga kauli ya Serikali kwamba wamekubaliana kusitisha mgomo wa walimu uliopangwa kufanyika Januari 9 mwaka huu.

  Jana Naibu Waziri Tamisemi anayeshughuliki Elimu, Kasim Majaliwa aliliambia gazeti hili kuwa mgomo huo umesitishwa baada ya Serikali kukutana na viongozi wa CWT Desemba 25 mwaka jana na kukubaliana wafanye hivyo.

  Hata hivyo kwa upande wake, Mukoba alipinga kauli hiyo ya waziri."Ni kweli tulikutana na Serikali lakini sisi hatukukubali kusitisha mgomo kwa sababu madai yetu hayajatekelezwa," alisema Mukoba.

  Alisema Serikali imekiuka makubaliano kwamba fedha za walimu zingelipwa kati ya Novemba na Desemba mwaka jana.Huko nyuma Serikali ilikuwa imekubaliana na CWT, kwamba fedha hizo kiasi cha Sh49.6 bilioni zingelipwa katika Novemba na Desemba lakini baada ya kufanya tena uhakiki ilibaini kuwa fedha hizo zimeongezeka hadi kufikia Sh52 bilioni.

  Uhakiki huo ulikamilika Desemba 2 mwaka jana baadaye Serikali ilitangaza kuwa fedha hizo zitalipwa kwa awamu mbili,Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Selestin Gisimba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, sababu za kusogeza mbele malipo hayo ni kutaka kufuata utaratibu wa makato ya kodi ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kupitia katika akaunti zao.

  "Tumeishagundua ujanja wa Serikali wamefanya makusudi kusogeza siku mbele ili walimu wafungue shule na mgomo uyeyuke lakini napenda kusema kwamba tayari ujanja huo tumeufahamu na kama ikishindwa kulipa fedha hizo mwezi huu shule hazifunguliwi,"alisema Mukoba.

  Alisema kwa sasa makubaliano hayo hayawezi kubadilika kwa sababu suala la uhakiki limeishamalizika na kwamba kinachotakiwa ni kulipa fedha za walimu.

  Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
  [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Comments


  +2 #12 BEBERU 2012-01-05 12:50 PIA NA MISHAHARA WAWAONGEZEE NA POSHO PIA ZIONGEZWE, HAKUNA KULALA SAFARI HII, SI MNAONA HALI YA MAISHA ILIVYOKUWA NGUMU, MADAKTARI TAYARI WAMECHARUKA NA NYIE PIA FUNGENI MKANDA MAPAMBANO YA HAKI MPAKA YAPATIKANE, NA POLISI PIA VIPI MBONA KIMYA? AU MMELIZIKA NA VIJIPESA MNAVYOPEWA? AU KWA KUWA MNAYO MIANYA MINGI YA RUSHWA NDIO MAANA HAINA NOMA KWENU?
  Quote
  +4 #11 kiboko 2012-01-05 11:27 Walimu shikamaneni kudai haki zenu,Wabunge toka 70,000 mpaka 200,000 tena kimya kimya wanatafuna fedha za nchi hii,Hivi huyu Mwalimu tunamchukiliaje ?!,Kwakweli Walimu baada ya Kulipwa madeni yenu sasa kinachofuata ni madai ya kima cha mshahara kivuke kiwango cha posho ya Mbunge kwa siku,maana huyu mbuge bila Mwalimu asingekuwa pale kwakweli mwalimu ni mtu muhimu sana na tunapaswa kumuheshimu kimaslai tuache ubabaishaji! KWAKWELI NAUNGA MKONO MGONO WA WALIMU WA TAREHE 9 .TUONE KAMA WALIMU WAKIGOMA MABOSI WATAENDA FUNDISHA.
  Quote


  +3 #10 baraka mushi 2012-01-05 11:21 jamani walimu tumuunge mkono mukoba,tujue tunaendelea kunyanyasika siku hadi siku,tumekuwa kama wendawazimu,hau dhaminiwi,we should have solidarity,let our decisions be the final,tugome!tu gome kwa pamoja,solidari ty 4ever!tukumbuke kwamba tuna madai mengi,kama waraka kandamizi!tusip osimamia haki zetu tutaendelea kukandamizwa!ka m we una taalumu yako,unaogopa nini kutetea haki yako!na njia sahihi sii nyingine sasa ni kugoma!chondech onde walimu tugome!
  Quote


  +4 #9 Neema 2012-01-05 11:06 Walimu tumechoka kunyanyashwa na mishahara yetu sasa uvumilivu umetuisha.Kifupi ni kwamba shule hazitafunguliwa mpaka tulipwe madeni yetu. Iweje pisa nyingi zitumike kusherekea miaka 50 ya Uhuru zikosekane zakulipa walimu?
  Quote


  +2 #8 NOAH MWASOMOLA 2012-01-05 11:02 SINA IMANI JUU YA SERIKALI YETU TENA, NA HILI HUWEZI NIBADILI MTIZAMO, MAMBO MENGI IME-PROVE FAILURE. Mwalimu ni kila kitu ktk dunia hii but serikali haithamini hili,TUMEONA KAULI HATA YA so-called RAISI ikiwa ni false defence on the issue,kama raisi mwenyewe kawasaliti walimu,nani atawtetea?naunga mkono mgomo kwa 100%, "TOGETHER WE CAN CHANGE THE WORLD" WALIMU WOTE TUSHIKAMANE.
  Quote


  -3 #7 jakob tuli 2012-01-05 10:46 NAKUUNGA MKONO WE KAWAMBWA, WALIMU MTAMBUE KUWA MKOBA SIO MTETEZI WENU,KUNA SIRI NAWAPA LEO,2015 ANATAKA KUGOMBEA UBUNGE HUKO KWAO,NOW ANATAFUTA UMAARUFU HANA LOLOTE MPUUZENI
  Quote


  +3 #6 osokoni 2012-01-05 10:27 Nawavowajua walimu wa Tanzania hiyo ni Tishia nyau shule zikifunguliwa utwaona kiguu na njia kupiga chaki kama kawa bila kujali wamelipwa au la watanzania wengi tumejaliwa sana kuongea lakini kutenda hakuna laiti tungeweza kutenda robo tu ya yale tunayosema hili taifa lingekuwa mbali sana, ngoja tusubiri tuone but iam doubtful!!!!
  Quote  +1 #5 chris nombo 2012-01-05 10:11 Tunadanganywa, hakuna uhakiki wala mgomo!
  Quote


  0 #4 chris nombo 2012-01-05 10:08 hizo ni danganya toto on both sides!!!
  Quote  -1 #3 kawambwa 2012-01-05 09:54 Mukoba ameshapewa chake, walimu mnapoteza tu muda wenu,kikubwa endelea kufelisha wanafunzi, vinginevyo haki haipo ndani ya serikali ya JK
  Quote  +2 #2 kashaija 2012-01-05 09:32 walimu mkilegeza msimamo serikali itaendelea kuwachea,km serikali ilipata mabilion ya sherehe za uhuru,iweje wakose za kuwalipa walimu?kazeni msimamo.
  Quote  +2 #1 Peter michael 2012-01-05 07:34 Walimu hachen woga ungeni mkono mgomo lasivyo serikali itaendelea kupiga danadana malipo yenu! swali dogo jiulizeni ni tangu lini madeni hayo yameanza kuakikiwa na kwanini hayalipwi? swala la serikali haina hela ni uongo mbona posho wanalipana! wake up!
   
 2. Mkiliman

  Mkiliman JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 957
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Hawa Walimu wa TZ waache wateseke kwani wao husema tu Tutagoma lakini wakitishiwa wote wanaenda kupiga chaki. Mimi siwaamini hata kidogo walimu wetu. Ukombozi ni ninyi wenyewe kuandamana au kugomea kazi, na endapo mgomo utafanyika hiyo ndio salama yenu, kinyume na hapo hizo 52 Billions hamtalipwa mpaka mwisho wa dahari..........!!!
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Walimu huwa hawana utaratibu wa kugoma,ukitaka 7bu ntakupa,
   
 4. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Viongozi wa CWT ni wanafiki, wanatumia kigezo cha migomo ili waonekane wanafanya kazi. Wameshindwa kutatua matatizo ya msingi ya walimu hasa mishahara midogo ya walimu huku wao wakijilipa marupurupu kibao.
   
 5. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,152
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Hawana jipya hao kwa sababu ndio wimbo na sala yao ya kila siku hiyo, kumbuka, usimwamini muongo hata kama atasema ukweli.
   
 6. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Na leo Mkoba amesema mgomo umesitishwa rasmi kwa hyo zilikua porojo za Mkoba na Oloch
   
 7. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #7
  Jan 6, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mr Zero si umeona walimu walivyo wanafiki? eti wamefuta mgomo hebu ona mkoba anavyo danganya walimu"Ni vyema walimu wote mjitokeze katika vituo vyenu vya kazi siku hiyo kwa maana kutokufika kwenu kazini kunaweza kutumiwa na Serikali kama kisingizio cha kutolipa madeni hayo kwa kigezo kuwa walimu wa kulipwa hawapo,"
   
Loading...