Hivi walimu ni wanasesere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi walimu ni wanasesere?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mchajikobe, Sep 1, 2009.

 1. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JF hivi mnaonaje hadhi ya hawa walimu ambao bila wao hakuna mmoja kati yetu angeweza fanya mengi tunayofanya sasa,je ni wanasesere ambao hakuna anayeogopa wachezea?au labda serikali inamatabaka ya waajiriwa wake,sababu kila mwaka malalamiko ya mishahara ni yao,hii serikali kama kweli imekumbwa na financial crisis na inajiamini kiutendaji,kwanini isifanye zamu zamu za kuchelewesha mishahara kwa kila waajiliwa wake?Mfano leo wanawacheleweshea walimu,basi kesho iwe zamu ya wanajeshi!!
  Inatia uchungu sana ni sawa na mzazi kubagua watoto!!
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli walimu hawapewi heshima na kutahminiwa ipasavyo katika sehemu nyingi tu duniani na wala si Tanzania peke yake. Leo hii mimi, kwa kiasi flani kikubwa tu, nisingefika hapa nilipo leo isingekuwa kwa walimu niliobahatika kuwa nao kuanzia chekechea mpaka elimu ya juu.

  Walimu wangu hao walinifundisha mengi kuanzia hesabu, kuandika, kufikiria, nidhamu na mengine mengi tu. Wanahitaji kuthaminiwa zaidi ya wanavyothaminiwa sasa.

  Siku ya mimi kurusha kofia yangu kwenye ulingo wa siasa walimu ndio watakuwa signature issue yangu. I love you all teachers. You are immensely appreciated.
   
Loading...