Hivi walimu ni wajinga au wapumbavu?

Hivi walimu ni wajinga au wapumbavu?

nasaluka

Senior Member
Joined
Jun 20, 2015
Posts
149
Reaction score
185
"Mjinga hujifunza mpumbavu hubisha "
Katika nchi yetu ya Tanzania kundi kubwa la wafanya kazi ni walimu, lakini kwa maoni yangu ni kundi ambalo halijitambui kabisa na ni kinyume na lilivyotarajiwa.

Kero kubwa kwa walimu sio serikali bali ni chama chao kinachiotwa (CWT) ambacho kipo kwa ajili ya kuwaplease walimu pale wanapokuwa na lengo la kudai maslahi yao kwa Serikali.

Na chama hiki kimewafanya walimu kama mazombi na mtaji wa maisha ya wachache wanaojiita CWT, na hata hivyo uzombi huo wa walimu unadhihirika siku hadi siku.

Kwani wapo walimu hawajui hata ofisi ya CWT katika wilaya zao na hata kazi ya chama katika maisha yake ya kazi lakini anakatwa mchango wa CWT,

Je, walimu ni wajinga au wapumbavu?
 
Mwalimu kupata huduma ya chama haina ulazima wa yeye kujua ofisi za CWT wilaya au mkoa. Kubwa ni kushiriki katika shughuli za chama tangu ngazi ya tawi (shule) hadi Taifa. Uwepo wa chama cha wafanyakazi ni kwa lengo la kujenga mshikamano na siyo kufahamu maeneo yalipo maofisi ya chama. Kasome vizuri ELRA NA. 6 OF 2004 uelimike. Unawaita walimu wajinga/wapumbavu!! Watake radhi ndg yangu.
 
Wakati nimemaliza kidato cha sita,nikiwa natafakari naangalia nikasomee nini cha kuisaidia jamii! Kuna Mwalimu mmoja aliniambia "kijana wangu ukiamua kua mwalimu maisha yako yote yatakua ni kuvaa suti moja tu na tai kila siku,kusubiria mshahara kwa ajili ya kulipa madeni,utazaa watoto wako wanne na kujenga kijumba kimoja cha vyumba vitatu basi na usubirie hela ya kustaafu" Mpaka leo sijafanikiwa kuipata vizuri kauli ya mwalimu huyo aliyekua amebakiwa na miaka 5 kustaafu alimaanisha nini.
 
Kwa kifupi: sio wajinga wala si wapumbavu.

Tatizo ni la kimfumo (systemic problem due to issues inherent in the overall system...)
 
Hii kitu sio kama anavyoeleza huyu ndugu, ukweli ni kuwa hawa CWT ni taasisi kweli inayoshughulika na walimu lkn sio wote kwnza ilikuwa lazma kujiunga na kuanza kukatwa lkn baadae walimu walianza kuhoji kuwa kama mifuko ya kijamii inakuja kushawish wafanyakaz wapya kujiunga ktk mifuko yao, kwann na cwt wasje kutoa elimu na kuvuna wanachama bdala yke wanalazimisha tu.

Basi baada ya kubanwa sana na walimu hasa wa shahada ya kwnza waliamua kufanya opption ktk kujiunga. Hivyo kwa sasa kuwa mwanachama wa CWT ni lazma ujaze fomu zao za uanachama na wala co utaratib wa zaman kuwa sku utakayopangiwa kituo cha kazi ya ualimu basi tayari unakuwa umeshakua MWANACHAMA WA CWT na utaanza kukatwa tangu mshahara wa kwanza.
 
Mkuu, mke wangu ameanza kukatwa kwenye chama hiki na hajajaza fomu yoyote yupo kwenye ajira miaka 3 na ameanza kukatwa mwaka huu.
 
Ndg yangu huenda ulikuwa na ushauri mzuri kwa walimu lkn kwa uandishi wako hakuna mwl au mtu mwingine atakaefurahia

ukweli unauma mkuu, lakini ili mgonjwa alone lazima avumilie sindano ya moto hata mimi walimu siwaelewi tuwaweke kundi gani
 
Hii kitu sio kama anavyoeleza huyu ndugu, ukweli ni kuwa hawa CWT ni taasisi kweli inayoshughulika na walimu lkn sio wote kwnza ilikuwa lazma kujiunga na kuanza kukatwa lkn baadae walimu walianza kuhoji kuwa kama mifuko ya kijamii inakuja kushawish wafanyakaz wapya kujiunga ktk mifuko yao, kwann na cwt wasje kutoa elimu na kuvuna wanachama bdala yke wanalazimisha tu.

Basi baada ya kubanwa sana na walimu hasa wa shahada ya kwnza waliamua kufanya opption ktk kujiunga. Hivyo kwa sasa kuwa mwanachama wa CWT ni lazma ujaze fomu zao za uanachama na wala co utaratib wa zaman kuwa sku utakayopangiwa kituo cha kazi ya ualimu basi tayari unakuwa umeshakua MWANACHAMA WA CWT na utaanza kukatwa tangu mshahara wa kwanza.

Mwalimu KAIJAGE alishakimbia jukwaa hili maskini, utajibiwa na nani?
 
Inawezekana una lengo zuri sana la kueleza kile kinachokukera au kutaka kujua kile usichofahamu na pia inawezakana hata unachotaka kukieleza kimekupotea. Labda naomba nikuulize swali moja; je, unafahamu matatizo ya walimu? au kwa mtazamo wako walimu wana matatizo gani kadri ya hisia zako?
 
Mtoa mada naomb nikuambie jambo kwamba kama kwel ni mcha Mungu waombe radh walimu kwa kuwa hizo lugha mbil ulzotumia si za kiungwana. usimdharau mwinzako kwa kaz anayofanya tunaish kwa kutegemeana kwa kila idara pale unapoona kuna mapungufu katika idara ya mwenzako una nafasi ya kushauri na si kutumia lugha mbovu kiasi hcho kwan hata Mungu sidhan kama inampendeza. mwenzako anatoa sadaka yake kwa kazi anayofanya kwa nini umtukane?

Wewe unafikiri kazi gan iliyo bora hapa Tanzania? Then utambue USIACHE MBACHAO KWA MSALA UPITAO. Kwa kwel lugha uliyotumia ni ya kukatisha tamaa lakini okay nakubaliana na falsafa inayozungumzia kwamba "hakuna kweli moja"
 
Nikweli kwa asilimia 100 na muunga mkono aliye toa thread hii!!! mimi ni mwalimu na kweli sisi waalimu tuna mapungufu kwenye ufikiri!!! hajamdharau mtu bali amesema ukweli mtupu!! CWT si chama cha waalimu bali nichama cha watu flani hivi na waalimu wote wanajua na tunaibiwa tunaona hii ni kwasababu zifuatazo;

1. wameanzisha kitu inaitwa service charge kama tanesco vile uwe umejiunga uja jiunga lazima ukatwe hela;

2.mwalimu anaichangia CWT miaka yake yote mpaka kustaafu lakini malipo yake ni tishert ya CWT kila mwaka!!!

3. wanadai wanatoa mikopo kwenye vikundi, mi huu mwaka wa 8 nipo kazini sijawahi kutana na mkopo wa cwt!!! cha kuuzunisha hata kutoa huo mkono wa pole mwalimu akifa bado ni mbinde!!!! napesa wanayo kata ni zaid ya 10000 kwa mwezi!!!

sasa angalia kiasi cha fedha kinacho katwa kwa mwezi kwa kila mwalimu zidisha mara idadi halisi ya waalimu !!! mfano shule yangu hapa tuna waalimu 60 ina maana mwezi mmoja cwt kwa shule yetu tu ina beba zadi ya laki 600000/= sasa jiulize tuna shulengapi nchi hii na waalimu wangapi nchi nzima utapata jibu!!!

wanajenga majengo wanayapangisha wanadai pesa hizo wanarudisha kwa njia ya mikopo nimejaribu kupeleleza sio mimi tu bali hata mikoa mingine nayo iyo mikopo huisikia kwenye tv!!!

ukweli nikua cwt nichaka tu la ufisadi, hakuna ubalisia wowote na wanacho ki preach nje kuwa wanatetea maslahi ya waalimu!!! bali wao kazi yao nikujipa vikao posho na tujisemina hasa kwa huku mijini na kuwasahau weeengi waalimu!!! sasa mtoa thread katumia lugha kali ili sisi waliimu tufunguke huupofu umetuzidi!!!
 
Wewe ni nani kwanza hata ufatilie mambo ya wengine? aka walimu & had uwaite wajinga. ulikuwa hujui kusoma ww sasa unafahamu ndo unawalipa walimu wako kwa matusi? respect kwa walimu kwa kujitoa kwao. we'r all your products.
 
Cwt ni zaidi ya chama tawala. Hawana huruma hata kidogo.
 
Back
Top Bottom