Hivi wadada mko je jamani? Mwanitisha.....!!

Mar 2, 2011
86
20
Hi ndg zanguni wana Jf.
Basi jioni ya leo nilikuwa na rafiki yangu, mara punde ikaingia msg kutoka kwa mchumba wake (wa kike) ikisomeka hivi "poa usijali mungu atakutangulia baby" ghafla rafiki yangu akabadilika ghafla naye kumuuliza kulikoni ndo akanionesha hiyo msg. Nikamuuliza tatizo ni nini si ni wife (maana amemsave WIFE) ndo kakutumia nini tatizo?

Akajibu "tuliwasiliana naye mchana ila msg inaonesha ni mazungumzo yanayoendelea, je tutakuwa tuko wangapi tunaitwa baby?" Nikamwambia calm down atakuwa amekosea na tena huenda alikuwa anamtumia msichana mwenzie au mligombana au ulishamkutaga na dalili ya kukusaliti? akajibu "hapana lakini... kwanini?"

nikamwambia "wewe mpigie simu mwambie tu nashukuru kwa msg yako nimeipata" na akakubali
na alivyompigia bint alikuwa hakujua kwamba alikosea na kuituma kwake ndo akamuuliza na kumuomba amfowardie iyo msg na kaka alivyomfowardia dada akasema samahani nilikuwa namtumia rafki yangu Loveness yuko njiani anakuja kumbe nilikosea ikaja kwako, pls baby..


SWALI LANGU KWENU WADADA NA HATA NA KWA WAKAKA PIA: IKIWA NI WEWE NDO YAMEKUTOKEA UNGEELEWAJE NA NINI UNGEKIFANYA? JE NINYI AKINA DADA NI VIZURI KWELI HATA KAMA WENYEWE KWA WENYEWE MNAITANA YALE MAJINA YETU YA SWEET, HONEY, MY LOVE N.K? JE MNATUFICHA NINI SISI WAPENZI WENU WA KIUME ENDAPO TUNAKUTA/KUPATA MSG KAMA HIZO ZILIZOTUMWA TO THE WRONG INTENDED NUMBA?
 
wanawake huwa hawana shida, wanaitana bby, mpz, darlin na majina yote......
Na sijaona chochote kibaya alichotuma huyo dada.....

Mwambie rafiki yako/wewe mwenyewe kuacha kucomplicate issue....
 
Weewe nawe wa kishumundu nini?sasa cha kushtusha ni nini hapo pyaa?hebu nipate cha asubuhi mie
 
Ge'ez; nawaita kwa majina hayo rafiki zangu wapenzi, mama, mwanangu, my nieces n nephews n so many more! It is a woman nature to be sweet!

Ila mume wangu akimuita hivyo mshikaji wake (wa kiume) itanishtua!
 
Kwa wadada nikawaida kuitana hivo, lakini inaweza kuwa ticket yakukudanganya wewe kuwa huyo ni rafikiyangu wakike tu, chakufanya jiamini tu mkuu "UKIMCHUNGUZA SANA BATA HUWEZI KUMLA NYAMA"
 
Kama umekubali kumuoa basi inaonyesha wazi kiasi gani unmpenda na kumuamini vyengine visikushughulishe..labda alikua anakutania, au kama hivyo amekosea number...
 
kama ikiwezekana wasiwe wanatuita majina ya sweetie,baby na mengine ambayo huwa wanawaita wasichana wenzao coz ni rahisi sana kuwasingizia wenzao pindi wanapofanya madudu!!!!!!!!!!!!!! hawa viumbe wana mbinu nyingi asikwambie mtu!!!!
 
Binafsi, sipendi kukurupuka. Kama ana mashaka, ni vzr kujipa muda na kufanya uchunguzi wa kina. Kuitana majina ya namna hiyo haigurantee kuwa dada huyo ana mtu mwingine.
 
kama ikiwezekana wasiwe wanatuita majina ya sweetie,baby na mengine ambayo huwa wanawaita wasichana wenzao coz ni rahisi sana kuwasingizia wenzao pindi wanapofanya madudu!!!!!!!!!!!!!! hawa viumbe wana mbinu nyingi asikwambie mtu!!!!

wasiwasi wenu tu!
 
Mie sikubaliani na watu wa jinsia moja kuitana sweet, darling, honey.
Khah, viwanda vya kukoboana ndio maana vinaongezeka.

Majina hayo ni only and only kwa mtu nina interest naye, tena opposite sex.
 
mimi naona kuna ukweli kwamba hamna cha ajabu LAKINI pia naona kama ni njia mojawapo ya wadada kutuzuga. MAANA unaweza kukuta kaseviwa JACKLINE kumbe ni JACKSON... then ndo katumia msg "usijali beib" n.k
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom