NIMPENDENANI
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 6,114
- 5,397
Habari za asubuhi wana Jamii Forums.
Mwenzenu kuna jambo linaniumiza kichwa naomba fikra zenu.Kuna mtoto wa shemeji yangu tunamlea tangu wazazi wake wafariki miaka 14 ilopita kijana sasa yuko chuo mwaka wa pili.
Jana jioni amekuja kuniomba anataka kuongea na mimi nikamwambia sawa, kikubwa kwenye maongezi nikutaka kuoa
Nikamuliza amejipanga vipi sababu bado anasoma kwanini asimalize chuo ndio akafikiria kuoa.
Nimemwambia kwa roho safi tuu sababu yeye anaishi kwangu na wadogo zake ndugu za wazazi wao waliwakataa nimewalea mimi na hakuna kitu sija wapa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu wasijisikie wanyonge.
Cha ajabu amekwenda kumwambia mume wangu kua simpendi na sitaki akae kwangu na mume anashikilia muache aoe eti mtoto akililia wembe mpe,imeniuma yule mtoto kusema hivi sababu hakuna nisicho jitahidi kwao yeye na wadogo zake.
Hata chuo school fees nalipa mimi leo nimekua simpendi, nimemwambia fikiria tena unachotaka kufanya.
huyo mke akiolewa nyumba yakukaa hana inabidi aje tena kukaa nyumbani.
Sielewi waungwana hebu nisaidieni, jee kumwambia subiri ni sawa au nimekosea.