Hivi usalama wa viongozi duniani wanapotumia magari ya wazi huwa uko wapi?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,694
149,917
Katika dunia ya leo yenye vitu "sophsticated" viongozi huwa wanajiamini vipi kutembea kwenye magari ya wazi?


Mtu mwenye nia mbaya na alietayari kwa lolote, katika mazingira haya anashindwa kufanya lolote?

Binafsi huwa siamini sana katika huu ulinzi wa viongozi katika mazingira kama haya ya mikusanyiko mikubwa ya watu bali huwa naamini hakuna watu wenye nia mbaya au wanaokusaidia kutukeleza uhalifu wao katika mazingira ya aina hii.

Kama kiongozi fulani aliwahi kurushiwa kiatu tena katika mkutano wa ndani sasa usalama wa uhakika katika mikusanyiko ya wazi huwa upo wapi?


Mimi naamini usalama ni pale kiongozi anapohutubia akiwa ndani ya jengo na wote waliongia wanakuwa wamekaguliwa kabla ya kuingia tofauti ma hapo mimi huwa naona ni mbwembwe tu.

Kuna mazingira mengine ni vigumu sana kumdhitibi binadamu mwenzio hasa kwenye mikusanyiko ya wazi hata kama kuna askari/walinzi wanaovaa nguo za kawaida.

Nakumbuka nilishuhudia msafara wa Rais Mstaafu wa Marekani,George Bush alipokuja Arusha hakuwa kwenye gari ya wazi lakini alikuwa akipunguia wananchi mikona kutoka KIA mpaka Arusha mjini huku kwa juu akiwa na escort ya helicopter ya polisi.
 
Watasema unachochea watu kumdhuru mkuu akiwa kwwnye gari ya wazi....
 
Back
Top Bottom