Hivi upigaji wa Selfies tunapokuwa Vijijini au sehemu zisizo na hadhi ni prohibited kwa Watanzania?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Huwa nashangaa sana hasa pale ninapowaona Watanzania wakiwa busy sana kupiga picha zao mbalimbali hasa zile za Selfies wakiwa maeneo mazuri mazuri ya mjini au mijini na wengine wakiwa huko Ng'ambo / Ulaya lakini sijawahi kuona Watu wanapokuwa ama Vijijini Kwao au zile sehemu zisizo na hadhi sana wakipiga hizo picha na kuzitupia katika Kurasa zao.

Je kwa Watanzania wenzangu hivi kupiga picha za Selfies tukiwa Vijijini Kwetu au zile sehemu ambazo tunaona hazina hadhi Kwetu ni Prohibited ( hairuhusiwi ) au ni sisi tu Watanzania / Waswahili tunaendekeza tu ushamba kama siyo ulimbukeni wetu.

Leo naomba nitoe ombi langu kwenu Waswahili wenzangu kuwa kuanzia sasa hebu tujitahidi basi hata pale tunapokuwa huko Vijijini Kwetu tuwe tunapiga picha za huko na kuzitupia katika Mitandao yetu na hata uhalisia wetu wa kimaisha wa kimaeneo na wenyewe pia tuwe tunauweka hadharani na kamwe tusijifanye kuwa sisi tuna maisha mazuri wakati kumbe kiuhalisia hali siyo hivyo.

Nawasilisha.
 
Kwangu zipo za Kijijini tena wakati navua samaki nikiziangalia nacheka sana. Na hapa mjini maeneo tofauti.
 
Back
Top Bottom