Hivi unawezaje kuishi na watu hawa ....

Hivi unawezaje kuishi na watu hawa ....

Katika maisha unakutana na watu wa aina mbali mbali wakiwemo hao uliowataja, ila ni rahisi kuwagundua maana hawajifichi hata kama atakuchekea, kicheko chake si cha furaha bali unafiki. Uvumilivu ndio suluhisho pekee na usimshirikishe mambo yako ili azidi kuumizwa na maendeleo yako.

Mie natamani niwaambie acheni unafiki hahahaha ...
 
IGNORE THEM AND LIVE YOUR LIFE.....

mwisho wa siku aibu inakuwa kwao
 
Bila hao kuwapo, jamii haijakamilika. Yawezekana makundi yote ya tabia ulizotaja wasiwepo, lakini % kubwa tunao iwe makazini, sehemu za ibada, familia n.k. Cha msingi don't let 'em anger u for they'll know that they've successfuly conquered u.
 
Fl1 dear hao watu wapo, tunao na wengine tunaenda nao kanisani njia moja tena wengine tunakula nao sahani moja. Maana kuna methali inasema kikulacho ki nguoni mwako. La msingi ni kuendelea na maisha yako, get busy busy busy with uaself, ignore them na ukiweza kaa mbali nao. Shirikiana nao kwenye maswala ya msingi tu (msiba, sherehe za kifamilia, n.k) vinginevyo fanya mambo yako bila kuwashirikisha. Maana kila utakachowaambia watakikosoa tu, hakuna jema kwao (dont share with them ua future plans, just suprise them). Kama gari walione tu unaendesha, kama nyumba utawaambia siku unayoamia n.k.

Zaidi sana muombe Mungu akusaidie maana wengine ni ndugu zetu wa damu.
 
hakuna jema kwao (dont share with them ua future plans, just suprise them). Kama gari walione tu unaendesha, kama nyumba utawaambia siku unayoamia n.k.

Zaidi sana muombe Mungu akusaidie maana wengine ni ndugu zetu wa damu.
ndio dawa pekee hila in my case huwa na delete completely
 
hawa wapo na watakuwepo siku zote cha msingi ni kuwapuuza!mi huwa nawaonaga kama chachu ya maendeleo maana huwa wananitia machungu hivyo naongeza juhudi za maendeleo ili waumie zaidi!
 
MAMA FL,
Maisha ni mapambano, Ni mapambano marefu, Challenges ni nyingi lakini ushindi uko katika Dhamira ya mtu Binafsi, Kuna nyakati ngumu sana ambazo unakwazwa na uwezi kubeba wewe binafsi, unaomba mungu akupe uwezo wa kushinda, maana katika imani kuna Taraja, na katika taraja kuna ushindi. Bila watu dunia haiwezi kukamilika, Kila mtu na jinsi alivyoumbwa, na pengine namna alivyoaribiwa au kuaribika katika fikra na mtizamo na mwisho tabia.Tabia ya mtu ni kama sura yake, haibadiliki.Unachofanya ni kujua namna nzuri ya kuishi na kila mtu huku ukizingatia tabia yake na mwisho ushinde.
 
Very simple binamu.
Kunywa pombe ya kutosha.
Unapokuwa na alkoholi ya kutosha kichwani maadui zako wanageuka kuwa marafiki.
Ndio maana wanywaji hatuna maadui. Take it from me.
 
MAMA FL,
Maisha ni mapambano, Ni mapambano marefu, Challenges ni nyingi lakini ushindi uko katika Dhamira ya mtu Binafsi, Kuna nyakati ngumu sana ambazo unakwazwa na uwezi kubeba wewe binafsi, unaomba mungu akupe uwezo wa kushinda, maana katika imani kuna Taraja, na katika taraja kuna ushindi. Bila watu dunia haiwezi kukamilika, Kila mtu na jinsi alivyoumbwa, na pengine namna alivyoaribiwa au kuaribika katika fikra na mtizamo na mwisho tabia.Tabia ya mtu ni kama sura yake, haibadiliki.Unachofanya ni kujua namna nzuri ya kuishi na kila mtu huku ukizingatia tabia yake na mwisho ushinde.

nakushukuru sana Renegee ...nafurahi sana kupata mawazo kwa watu tofauti tofauti mawazo yako ni mazuri sana na ya ukweli
 
Very simple binamu.
Kunywa pombe ya kutosha.
Unapokuwa na alkoholi ya kutosha kichwani maadui zako wanageuka kuwa marafiki.
Ndio maana wanywaji hatuna maadui. Take it from me.


hahahah Binamu na ushauri nasaha ..mwingine anaweza kumwaga pombe yako makusudi tetetete unafanyaje kama i kurusha ngumi ya mlevi
 
kwakweli hawa watu wapo na kadri dunia ingalipo watakuwepo na kwa upande wangu nawapenda wote kwani cha kwanza ishi kanakwamba hawapo, usisikilize maneno yao jifanye usikii then ishi vile unapenda as long umkwazi mtu alafu wape suprise marazote wasijue mipango yako labda ile ulonauhakika nayo maana biblia inasema waandaa meza mbele yangu machoni kwa watesi wangu na kikombe changu kimefurika so tunawaitaji hawa watu sana ili watushangilie tutakapofanikiwa ni kibibilia kabisa
 
My dear, mengi yamependekezwa lakini cha MUHIMU zingatia usemi usemao: ADUI MPENDE! Utakayemuona ana kasoro yoyote juu yako, muonyeshe upendo. Kwa ujumla tabia yako iwe nzuri kwa jamii inayokuzunguka, i.e.
- Mkarimu, unapenda kusaidia wenzako
- Mpole,
- Mkweli,
- Mcha Mungu
- Mtumia busara katika kushauri watu
n.k.
Hapo utakuwa UNASEMWA VIZURI na kila mtu, hivyo hata wenye tabia hizo utaishi nao vizuri, na zaidi unaweza KUWABADILISHA kutokana na ukarimu wako.
 
Huo ni mtihani mkubwa hasa inapotokea watu hao ni ndugu wa kuzaliwa nao! Na inakuwa mbaya zaidi kama wo wamekuzidi umri wewe ni mdogo, unaweza kunywa sumu,....wanajua jinsi ya kukuchanganya, wanakutafutia maadui kila siku! yaani wao wanafanya bidii dunia nima ikuone mbaya! ukiwa mzembe kwa kujifanya eti unawapuuza tu watakuangamiza! amini usiamini mimi jipange la sivyo....
Ni mbwa, wanyama, mashetani na takataka kabisa, ila kwasababu tunaishi nao hamna kukaa kimya, pigania haki yako ya kuheshimiwa ikibidi hata kwa "ncha ya panga"! maana si wakati wote diplomasia inafanya kazi...na wahenga walisema amani haipatikani ila kwa ncha ya panga.
 
Back
Top Bottom