Hivi unaweza kumpata Mpenzi bila kutumia Fedha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi unaweza kumpata Mpenzi bila kutumia Fedha?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by mmaroroi, Jun 26, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa hali ya sasa pesa inatangulizwa sana katika mapenzi japo kwa kununua soda au zawadi ndogo au kuweka Vocha kupiga simu.Unaweza kumpata mpenzi kwa sasa kwa kuongea tu bila kutumia fedha?
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Kabisa kabisa....inetegemea unazungumzia pesa katika muktadha upi...kama ni sehemu ya gharama za kumpata, kwa maana ya usafiri, mawasiliano nk hiyo ni kawaida na huwezi kusema umetumia fedha kumpata...fedha ninayojua mimi ni ile ya kuhonga, au kwamba lazima umnunulie labda gari au kitu cha thamani ndo uone ndani. Mimi hiyo sijawahi kufanya.
   
  Last edited: Jun 27, 2009
 3. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Ndugu zanguni mwanamke ni bidhaa adimu hujawahi sikia hivyo!!kama wewe huwezi tumia hela kumhandle umekwisha watakutafunia mpaka ukome na ubahiri wako.
   
 4. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tuelimishane mbinu mbalimbali zinazowezekana kutumika kwa hilo.
   
 5. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Huwezi kumpata labda utupe mbinu!!yaani hata messagi usitume.hii sijawahi sikia kwa kweli.
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo ndio kusema kama huna fedha ndio basi tena kwa mapenzi?
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mbona kuna jamii ukimhonga mwanamke anaona kama umemdharau,hivyo unamnunua,hiyo imekaaje?
   
 8. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  hakika jaribu kuchunguza mkuu
   
 9. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #9
  Jun 27, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo si kweli kwa upande wangu. My wife sikumpata kwa kumwaga fedha. Nilifanya nae mazungumzo tu na hatimae nikajenga uaminifu...vitu vikafuata baadae (if you know what I mean)...na sasa ni 14 years later....Mambo bado safi....
   
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Jun 27, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Bila fedha hukosi mapenzi tu hata pa kuishi, chakula, marafiki hupati. Huu ndio ukweli, kaza buti kiongozi maisha sio lele mama!
   
 11. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #11
  Jun 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Gharama za mawasiliano hazikwepi kwa kumpata dada..kwa kuwa utawasiliana nae..vipi..kama hamna mawasiliano...

  Gharama nafikiri anazo zungumzia jamaa hapo juu ni mnatoka kwenda nae dinner,lunch inabidi umtoe pesa ya nauli..au "utasikia nikifika kituo flan nachukua tax uko wapi"
  Akifika hapo anakupigia niko nje hapa.....unakuta hata hajashuka kwenye tax...ulipie kwanza...kwanza itabidi ujiongeze...

  Wakati wa kuondoka napo....inabidi umtoe pesa ya tax au nauli..na hiyo ina range from 5000 - 20000.Kwa kuwa kashakuonyesha shida toka anapo kuja..kwa kuamua kupanda tax wakati hana uwezo wa kuilipia.Hatuwezi kukwepa wengine unaweza kujitambulisha kuwa unafanya kazi au ukampa bussness card yako.....akisha pata card hiyo basi yeye anaangalia hiyo card na si wewe tena anajipanga namna hiyo.

  Kwa maisha ya sasa hatuwezi kukwepa kijitambulisha kwa watu nini unafanya.Sasa wewe unakuwa na intension nzuri yeye anajipanga kulinga na title..kazi au kipato.
  Wengine ana kazi yake lakini hata nauli ya kuja kukutembelea mpenzi wake..inabidi umtumie....anakuja mkavu mkavu tu...na pochi...au begi na nguo mbili.Sasa hiyo inakuwa ni one way love...yaani yeye haingii gharama kukupata ziadi ya kiuno chake.

  Mwisho wa siku wanasema wametumiwa na kulalamika kuwa wanaume wamezaliwa na mama mmoja wanafanana wote...atleast hata kama una shida kuwa na moyo wa vita..mwambie hata niko busy na kitu kingine...kesho ukipata nauli umtafuta na wewe...sio yeye kila siku ndio wa kukufata..na kukurudisha..siku asipo kufata walalamika.

  Yaani sijui nazeeka au vipi hizi gharama za wazi wazi ...ni balaaa
   
 12. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #12
  Jun 27, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  kuna wanawake nimekutana nao..ni wadada wasomi na wenye hekima zao na kazi zao na pesa zao...lakini wanamsemo mmoja.."kila siku tunaspend more than 2 hours looking pretty for you guys, we deserve the free drinks, rides and offers"

  bila hela kwa maisha ya sasa sijui utamdanganya nani..kila mtu anaweza kutoa maneno matamu then what? from personal experience nimegundua ata wife wangu nisinge tembeza lunch offers, dinner offers, covering drinks in the club..NISINGEMPATA!!

  Ps: the days of handsome boys are long gone! unaweza mega but thats abt it..lakini kama unahitaji mwanamke wa kukeep, utaachwa tuu kama hauko safi!
   
 13. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #13
  Jun 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Vjjana siku hizi mna shida kweli kweli. Enzi zetu ilikuwa ni mapenzi ya kweli, hakuna pesa, wala una cheo gani au mtoto wa nani. Siku hizi mpaka uwe na pesa? Poleni sana.
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu huwezi yaani nakataa kata kata waswahili wanasema mkono mtupu haulambwi.
  Anaye bisha jaribu kumtokea mrembo omba namba zake za cmu kisha uwe una mbipu akupigie umtongoze uone kama itawezekana....
   
 15. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Andika maumivu tu hapo! Ila akibipu yeye wewe piga na mwengezee salio.....lazima uingie Uvinza na kujiexpress!
   
 16. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #16
  Jun 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahahaha hii nimeitumia sana si unajua ugonjwa wa mashori ni salio mimi akibip nakwea hewani sijalishi kapib kwa voda au zain namalizia kuwa ngoja nikuongezee salio namtumia buku 5 aaaah mzee mbona sms za kumwaga tu kila wakati mala umekula ooh umeoga yaani kero tupu week end namtoa hapo sijatamka chochote wewe uncle Masa utakuwa unaangalia kivuli tu.
   
 17. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #17
  Jun 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  No, huwezi kupata mazee..Hivi yaonekana huijui vyema dhana ya uwekezaji..Hivi toka lini visivyopandwa vikavunwa?
   
 18. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #18
  Jun 27, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahahaha hata wao wanapo mtongoza mwanaume wanatumia pesa kukushawishi uingie kwenye anga zake.
   
 19. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #19
  Jun 27, 2009
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Ni sawa na unapokuwa unatafuta kazi lazima uingie gharama za printing, transport etc. Huwezi kusema uliingia gharama kupata kazi kwa maana ya kuhonga. Gharama za muhimu ni lazima utaingia tu. Jamani hata kumtoa out ili upate wakati muafaka wa kuuza sera zako hamna? Ila usijifanya kujionyesha unatumia sana ili kumpata maana atavutika kwa pesa yako na siku zikitoweka ndo utabaki kumsikia redioni!
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Jun 27, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Inaonekana dhana ya uwekezaji unaielewa kwa kina... :D
   
Loading...