Jindal unatisha....Zamani kaseti hizo zilikuwa zinatumika katika vibanda vya pombe ya kienyeji. Muuza pombe alikuwa anachukua hiyo tape alafu anarekodi vipindi vyote hadi taarifa ya habari, wateja wakishafika kuanza kulewa usiku unapozidikuwa mwingi anachukua redio yake na kutia tape, ngoma inaanza kulia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, kwa kuwa pombe imesha controll celebrum walevi hudhani saa mbili usiku kweli na kuendelea kulewa.
Hizo enzi hizo unazipata kwenye maduka ya RTC tu na lazima upewe na chumvi au vikombe vya kioo....
Hiyo rewinder kwetu ilikuwa marufuku kuitumia, eti inamaliza betri.mie nakumbuka enzi hizo nyimbo kama imeisha unataka kusikiliza tena inabidi utumie peni kurewind kama rewinder ya radio imekufa... hahahaha
Ule upande ambao "Mkanda" wa kaseti ndio upo full tairi huzunguka pole pole na ule upande ambao ni empty huzunguka kwa Spidi zaidi, yaani kama una play kaseti From side A kwenda side B basi side B tairi litazunguka kwa spidi zaidi,ni kwaajili ya "Load" tu.Nnachokumbuka ni kwamba kwangu nilikuwa najiskia raha sana ikiimba huku naitazama kuliko kucheza.
Swala lililokuwa linanichanganya ni kwanini wakati flani tairi moja kwenye kanda linazunguka speed sana kuliko lingine.
Pole sana Mkuu.Mwaka 1998 nilirekodi mazungumzo yetu mimi na mchumba wangu kwa kutumia Radio yangu aina ya HITACHI. Ule mkanda (cassete) ulikuwa na muziki wa bingwa wa Soukous Alain Kounkou wa Zaire(Congo DR) sote tulikuwa tukipenda sana kusikiliza rekodi zake huyu nguli. Mchumba alikasirika kwa kurekodiwa bila ridhaa. Niliamua kununua mkanda mwingine kama ule tena, na ule wenye sauti yake nikauhifadhi ktk shubaka la makorokoro ambayo kwa kawaida si muhimu sana wala si takataka, Hayatupwi. Mwaka 2000 tuliowana na kuj'aliwa mtoto. Kwa mapenzi yake MUNGU mke wangu alifariki mwaka 2011 akiwa mjamzito wa mapacha wawili na niliwapoteza wote. MUNGU ni mwema mke wangu aliniachia Bint yetu wa kwanza aliyezaliwa mwaka 2006 na wakati mama yake anafariki alikuwa na miaka mitano sawia. Juzi huyu bint yangu ametimiza miaka 10, niliamua (sijui kwa nini) kumuuliza kama anakumbuka chochote kuhusu mama yake akasema hakumbuki vema. Niliamua kuchukua ile Radio na ile cassete na kumuomba tuisikilize. Tulilia sana! Ubarikiwe mtoa mada.
Umenikumbusha mbali sana wakati huo betrii zikiisha hazitupwi. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Mkuu hii sio panasonic kweli?Hizo enzi hizo unazipata kwenye maduka ya RTC tu na lazima upewe na chumvi au vikombe vya kioo....
Ni panasonic spika moja pia zilikuwepo spika mbiliMkuu hii sio panasonic kweli?
Halafu kulikua na lile tangazo la biashara kupitia RTD idhaa ya biashara...Ni panasonic spika moja pia zilikuwepo spika mbili