Hivi unakumbuka nini ukiona picha hii??

Hivi unakumbuka nini ukiona picha hii??

Muuliza swali kauliza swali techinical sana. Sababu majibu yake lazima yatokane na mikondo miwili. Yaani historia pa1 na sayansi na teknolojia.
Kanda,tape cjui nn,sawa lakin zilitumika miaka gani,ubora wake na ubaya wake kabla ya cds ambazo nazo tayari zimepitwa na wakati.
uzuri wa tape Inadumu kidogo ila cd ikikwaruzika ndio basi tena
 
mie nakumbuka enzi hizo nyimbo kama imeisha unataka kusikiliza tena inabidi utumie peni kurewind kama rewinder ya radio imekufa... hahahaha
Sio rewinder kufa, kubana matumizi ya betri zisiishe haraka
 
Pale mwanza mitaa ya makoroboi utakuta msukuma keshauza ng'ombe zake kanunua inaweka kanda ya hesabu gharama, miziki ya kilimambogo na katitu ya kenya, acha si mchezo redio imewekwa begani anakata nayo mtaani
 
Yekeyeke, Dunia hii mama lukumbalukumba, mukomboti, thank you Mr. DJ for playing my song, Ohhh mesenja..... naam boss
Aaah, kilimambogo na katitu, na less wanyika, shemeji agness na afro mtoto wa sagana
 
Nakumbuka mambo yakurewind unashikilia button kitu kinazunguka weeeeee dah" ad uipate nyimbo inapoanzia shughuli
 
mie nakumbuka enzi hizo nyimbo kama imeisha unataka kusikiliza tena inabidi utumie peni kurewind kama rewinder ya radio imekufa... hahahaha
Those were the days when men were men and girls were still virgins
 
Zamani kaseti hizo zilikuwa zinatumika katika vibanda vya pombe ya kienyeji. Muuza pombe alikuwa anachukua hiyo tape alafu anarekodi vipindi vyote hadi taarifa ya habari, wateja wakishafika kuanza kulewa usiku unapozidikuwa mwingi anachukua redio yake na kutia tape, ngoma inaanza kulia taarifa ya habari ya saa mbili usiku, kwa kuwa pombe imesha controll celebrum walevi hudhani saa mbili usiku kweli na kuendelea kulewa.
Hah hah hah hah, sawa bwana mkubwa. Nimeshikilia mbavu kwa maumivu ya kicheko
 
mie nakumbuka enzi hizo nyimbo kama imeisha unataka kusikiliza tena inabidi utumie peni kurewind kama rewinder ya radio imekufa... hahahaha
Pen ya Bic ndio ilikua maarufu kwa ku rewind hizo Kaseti.
 
Nakumbuka ilikua Mkanda wa kaseti ukikatika unaunganisha na zile gundi za karatasi au plastiki "Masking tape"
 
nakumbuka kurekodi nyimbo zangu kwenye kanda.
 
Kuna ile style ya kujirekodi sauti kwenye hiyo Kaseti,mnawatumia salamu ndugu zenu wanaoishi mbali kwa kujirekodi sauti zenu kisha kaseti mnampa anayesafiri kwenda huko wanakoishi jamaa zenu ili awapelekee waisikilize.
 
Back
Top Bottom