Hivi unafahamu siku moja utakufa?

Kufa kunatisha japo sina experience ya kufa, kuna siku naweza kujikuta nawaza juu ya kufa hua nakosa raha kweli kweli.
Napenda siku nikifa niwe nimemaliza kazi ya kuwasomesha watoto wangu na wana maisha yao.
umeongea kama mimi ninavyo waza
 
Mdogo wangu kabla ya umauti alilazwa hospital ,wakati yupo hospital alikuwa anahofu sana ya kifo nasi tulikuwa waoga Wa kumpoteza .Tulikuwa tunalala hospital huku tumemkumbatia kwa zamu zamu mpaka manesi wanatufukuxa tunatoka njee tunavizia kuchungulia dilishani huku machozi yakitutoka sababu alikuwa anatuita kwa majina kwa sauti kubwa tumshike Japo mkono.lakini wakati ulivyofika alifariki akiwa na oksijeni na macho haoni ata kunishika mkono akuweza yaaniii daaahha! KIFO CHA UCHUNGU NA AKIZOELEKI
 
Ukiwa mcha Mungu kifo ni kama one way long distance flight.
 
Sijawahi kuhofia kufa kwa kweli " ila nachoomba siku ya kufa kwangu kusiwe kwa mateso na kuteseka sana

Sent from my TECNO-C5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hiyo mistari ya mwanzo (juu) umeandika kwa ujasiri sana kama vile unaona kifo ni jambo la kawaida, nakuhakikishia kifo hakizoeleki ndio maana miaka nenda rudi watu wanalia msibani, hayo maneno ya ujasiri yanatokana na kwamba hauumwi wala hujaona dalili ya roho kuacha mwili.

Niwe mkweli tu mimi naogopa kufa kinoma tena nikikumbuka kufa nakosa raha mno.
 
Acheni ujinga. Mrudieni Mungu. Unawaza kitu ambacho hata ufanyeje huwezi kuzuia ikifika siku yake. Inatosha kuwaza leo yako na chochote ambacho mkono wako uliwezalo kufanya, lifanye kwa nguvu zako zote, kwa akili zako zote na kwa moyo wako wote. hayo mengine acheni kumsaidia Mungu. Mungu hasaidiwi. Hata hao watoto unaosema uwasomeshe, hata ukisomesha bado utakufa tuu. Hata usipowasomesha bado watasoma tuu kama ni mapenzi ya Mungu
 
Nilikua naogopa zamani ila sio sasa, ila nikifikiria kukaa kaburini mwenyewe natamani tuzikwe wawili ha ha ha

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
 
One day Yes...kwa maana imeandikwa kila nafsi itaonja mauti
 
Pole sana ndugu.. kifo hakizoeleki hata kidogo.
 
Nilikua naogopa zamani ila sio sasa, ila nikifikiria kukaa kaburini mwenyewe natamani tuzikwe wawili ha ha ha

Sent from my SM-J700H using JamiiForums mobile app
Hata mkizikwa wawili still hamtambuani wala hakuna anayeweza kuamka na kumwambia mwenzake kitu.
 
Hahahahaaaa.. unaweza kujikuta machozi yanatoka unapokumbuka kifo..
 
Uliumbwa bila kuhoji wala kuomba basi usimpangie kazi aliyekuumba..
Kufa kupo tu cha msingi tenda mema uwapo duniani ili ukaishi vema huko uendako.
 
Sawa mkuu
 
Death is not my business and i never worry about it, becouse it comes when i do not know! !
 
Mwanangu kufa kunauma sana


Ni maneno ya mama yangu mzazi siku chache kabla ya kuaga dunia.

Sent from my Bravo Z11 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…