Hivi ukiwa nje ya mfumo wa siasa ya chama cha mapinduzi huwezi ku-run maisha yako?

huko kwenu vipi

JF-Expert Member
Jun 4, 2015
1,519
1,462
Habarini wanajamvi...

Hivi ukiwa nje ya mfumo wa siasa ya chama cha mapinduzi huwezi ku-run maisha yako binafsi?

Hivi kwenda chama chochote si ni haki ya kidemokrasi??

Kutoka chama Fulani kwenda chama kingine,si ni haki yako kidemokrasia?

Kutoka ccm kwenda chadema,ukatoka chadema kwenda CUF,na ukitaka kutoka CuF kwenda CCM tena ni lazima uombe radhi? si ni haki yako kidemokrasi kwann uombe radhi?? huoni unajidhalilisha??


Hii inanikumbusha kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,aliyewahi kusema sina pakushika,nimekosa mm nimekosa mm nimekosa sana hivi watanzania nani katuloga???

Unaomba radhi ili iweje?

Hawa wote wanaoomba radhi kwa Magufuli,wote Magufuli atawaweka wapi??


#Fredy_mpendazoe siku hizi mbona simsikii? baada ya kuona hapewi nafasi ameamua kukaa kimya??

#Jerry_muro nae ameamua kukaa kimya??

#Mosses_Machali nae amekaa kimya??

#Yule_wa_Baki_madarakani nae ameamua kukaa kimya?

Kwann tunajipendekeza kiasi hiki? hivi mbona wazazi wetu hawajasoma na hawajajiriwa popote pale na wana-run maisha yao vizuri tu?????

Vijana tunashindwa kuendesha maisha yetu tukiwa nje ya mfumo wa siasa cha chama cha mapinduzi???

Unahisi baada ya wewe kukihama chama uliwaumiza wanachama? sidhani kma waliumia kiasi hicho kuomba radhi unajidhalilisha tu wala hakuna mwenye time na wewe!

Hivi ukiomba radhi then uongozi wa chama ukakaa kimya wasikujibu utajisikiaje???

Watanzania Mungu atusaidie....
 
Siasa ni uongo, wanasiasa ni waongo. Wanamsoma mtu, halafu wanautumia udhaifu wake kujinufaisha.
 
Kuhama chama ni haki yako, lakini kuendesha maisha ya kisiasa ukitegemea makombo lazima itakugharimu. Kwa mfano kuna watu waliishi zaidi ya miaka 20 wakitegemea safari ya matumaini. walinunuliwa chakula, mavazi, kulipiwa pango, ada za shule za watoto wao nk. Matumaini yao yalipokwazwa na vikao vya chama furani wakaelekeza nguvu kwenye safari ya mabadiliko, huko nako wakagonga mwamba. baada ya kugonga mkenge aliyekuwa akiwafadhiri naye akawachoka, waende wapi? Mkuu kama unahamia kwenye chama furani kuendesha siasa, hutajuta wala kumuomba radhi yeyote, utakabiliana na changamoto zote utakazokutana nazo. Lakini kama ulimfuata furani ukitegemea akishinda utapata cheo hiki ama kile, mkishindwa kutimiza malengo yenu ya ushindi, lazima uonje shubiri, haijarishi una PhD au ngumbaru. Kitakachufuata ni lazima utamuomba radhi kila mmoja, ikibidi hata mende wa ofisi ya chama husika ili upate huruma
 
Ulietoa maada una akili nyingi huwa najiuliza sana watu wanaoendesha maisha kinafiki kujifanya napenda sera kumbe matummbo tu.
Huwa nawashangaa wanasisa na hawa sijui polisi au usalama wanao jikimu kwa kufanya kazi ya kuua watu wasio hatia kwa kutumwa n.a. binadamu wenzao kwa maslai yao,kisa mshahara.Mbona watu wengi wanaishi bila ajira za ajabuajabu kama hizi na unafikinafiki na wana maendeleo kuliko wewe unaye unaishi kwa dhambi.
 
Ulietoa maada una akili nyingi huwa najiuliza sana watu wanaoendesha maisha kinafiki kujifanya napenda sera kumbe matummbo tu.
Huwa nawashangaa wanasisa na hawa sijui polisi au usalama wanao jikimu kwa kufanya kazi ya kuua watu wasio hatia kwa kutumwa n.a. binadamu wenzao kwa maslai yao,kisa mshahara.Mbona watu wengi wanaishi bila ajira za ajabuajabu kama hizi na unafikinafiki na wana maendeleo kuliko wewe unaye unaishi kwa dhambi.
 
Wengi huwa kwenye kundi kama nyumbu na hubebwa na mfumo. Hawana akili na uwezo binafsi, ni waoga na tegemezi kwa njia zote, ni vibaraka wasiofaa jamii kwa lolote.
Umasikini wa taifa una uhusiano wa moja kwa moja na aina hiyo ya watu kupewa nafasi za uongozi.
Tunahitaji viongozi wenye msimamo, wanaowaza kupambana kwenye shida na raha, kupita kwenye milima na mabonde bila kukata tamaa.
 
Back
Top Bottom