Hivi tuna wahariri kweli ?

Hivi tuna wahariri kweli ?

Avocado

Member
Joined
Aug 23, 2010
Posts
97
Reaction score
4
Siku chache zilizopita ilikuwa sikukuu ya vyombo vya habari,na katika siku hiyo kubwa liliozungumzwa ni uhuru wa vyombo vya habari,kwa kweli tunapenda vyombo vya habari viwe huru,lakini uhuru huo usitumiwe kupotosha jamii ili wanahabari wajinufaishe kwa kuuza habari zisizo sahihi,mimi hakuna jambo ambalo ninaliona kuwa ni kero kubwa kama suala la TAKWIMU.Linapotokea jambo lolote ambalo litahusisha idadi ya watu au vitu,ndipo utakapo ona jinsi ambavyo wahariri hawako makini.kwa mfano jana magazeti ya mwnamchi na Tanzania daima yalitoa takwimu za watu waliopata kikombe cha babu kwa tofauti ya ajabu,gazeti moja watu milioni tatu,na lingine likiwa na watu laki tatu.Hakuna siku ambayo takwimu zitakuwa sawa kwa vyombo vyetu vya habari hapa Tanzania,sijui waandishi na wahariri wetu wamefundishwa kuchakachua kila kitu ? Hii inasababisha sisi wananchi tunategemea kupokea taarifa mbalimbali toka kwenye vyombo hivi vya habari tukose imani na habari tunazozipokea,Kuna haja kwa vyombo vinavyosimamia tasnia hii kuweka sheria kali kwa vyombo vinavyopotosha wananchi,kwani wanatulisha sumu,na kutufanya wajinga,kwa kutupa habari zisizokuwa sahihi.
 
Back
Top Bottom