Hivi TTCL wamefilisika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi TTCL wamefilisika?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mchokozi, Feb 27, 2012.

 1. M

  Mchokozi JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba mwenye taarifa za ndani zaidi anifahamishe kwani sielewi mwenendo wa Kampuni Komgwe ya mawasiliano nchini (TTCL), nimesitushwa na kuona kwamba maeneo mengi yanayopata huduma ya simu za mezani kama Magomeni, Wageni, Osterdbay nk kwa hivi sasa hayana huduma hii. Mimi naishi Magomeni nilipofuatilia niliambiwa kuwa TeS sijui kitu gani haifanyi kazi,na nilipouliza itapona lini niliambiwa haijulikani na wala hakiponi ila wanabadilisha kwenda kwenye TeS nyingine na kwa sisi wateja wadogo simu zetu hazitaweza kupona, je suala hili ina maana walikuwa hawalijui? au TTCL wamefilisika kiungozi na Ufundi? Na kibaya zaidi tetesi nilizozipata nimeambiwa wafanyakazi walikuwa wanategemea kulipwa mshahara wa mwezi february leo 27/02/2012 lakini hata Salary Slip bado hazijatolewa. Mweye taarifa atufahamishe la sivyo je Hivi TTCL wamefilisika ??????
   
 2. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,733
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  TTCL ni miongoni mwa mashirika mengi ya umma yanayopumua kwa mshine. Mengine ATCL (ambalo limebaki jina tu!), UDA (ambalo kila mtu amechukua chake hata parking).....
   
 3. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kufilisika? Hii haiwezekani. Shirika hili ni la wasauz. Huduma wamezidiwa. Mashirika ya simu za mikononi ndiyo yanawazidi. Lakini hawawezi kufilisika.

  Ni wajanja sana. Wanakula ki simba mwenda kimya. TAFAKARI.
   
 4. I

  INTELLECTUAL AT WORK Member

  #4
  Feb 28, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tatizo linaloikumba TTCL ni management mbovu usitaka kuangalia maslahi mapana ya nchi, wachache wanaihujumu shirika hili na kuonekana kuwa kama shamba la bibi.ukirudi nyuma utatambua kuwa TTCL ni miongoni mwa mashirika ya kwanza tena kwa industry ya mawasiliano ilikuwa ni ya kwanza Tanzania na ilifanya vizuri hapo nyuma,ila baada ya madeni makubwa ya liosababishwa na taasisi za serikali ambazo hazikuwa tayari kulipa gharama ya matumizi ya simu kulingana na matumuzi yao ndio iliyoifikisha TTCL hapo ilipo, pili kuingia kwa makampuni mengine ya simu Tz ni Miongoni mwa sababu ziliopelekea TTCL kufikia hapo ilipo sasa, japo walikuja kushtuka kuanzisha simu za kiganjani kwa kuchelewa, sasa wamekuwa mzigo kwa serikali na kwa walipakodi
   
 5. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #5
  Feb 29, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mi niliwachukia sana simu yangu ya mezani nimeripoti ubovu tangu Jauari 28 mwaka huu na baadae tarehe 2,7, na 9 Februari lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika. Kama wanalipwa mishahara ni kwamba wanatuibia kodi zetu watanzania..
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mali ya umma!
   
Loading...