Hivi thamani ya maisha ni nini?

Duh!!!
 
Ni kumtukuza na kumuabudu Mungu,kwani alituumba ili tumuabudu...
Bado sijaelewa umuhimu wa kuishi hapa duniani.
Wapo wanaofurahi, wapo wanaoteseka na wengine wapo wapo tu.
 
Thamani ya maisha ni wakati amani inapoanzia kwenye akili 'peaseful mind'
 
...hatukuumbwa sisi wala majini (viumbe) ila tumwabudu yeye muumba..
Mm naamini kuna kusudio kubwa LA kuumbwa viumbe vingi kisha mwanadamu pekee akapewa akili ya kujitambua na matamanio ya kutamani pamoja na uhuru wa kuamua,bila shaka ilo kusudio ni kujaribiwa kwa matendo yetu na swala LA kutofautiana yule hana uyu anacho au uyu ana furaha yule hana ni sawa na wanafaunz wanapokuwa kwenye chumba cha mtihni nikawaida kuona wengine wanafuraha wengne hawana wengine wpo full mandaliz kila ktu wanacho wengne ata peni anaazia kwenye chumb cha mtiani na ayo yote ni Uhuru WA MTU kuckuchagua.

So kuwa na furaha au uzuni\kuwa nacho au hauna ni uchaguz.WA mtu kwasabbu.lengo LA Muumba ni kumuabudu yy tu
 
Bado sijaelewa umuhimu wa kuishi hapa duniani.
Wapo wanaofurahi, wapo wanaoteseka na wengine wapo wapo tu.

Furaha ni very subjective mkuu na Mwenyezi Mungu katujalia namna alivyoamua yeye ili kutujaribu. Wengine kawapa maisha mazuri, wengine ya kati na wengine ya dhiki kabisaa. Kikubwa ni kumuabudu yeye ndipo tutapata furaha.
 
Bado sijaelewa umuhimu wa kuishi hapa duniani.
Wapo wanaofurahi, wapo wanaoteseka na wengine wapo wapo tu.
Maisha hayana maana zaidi ya kutimiza wajibu tuliopewa na Mungu wa kuzaliana , kulea watoto, kumuabudu Mungu. Kiukweli maisha yetu yana maana zaidi kwa muumba mwenyewe kuliko sisi viumbe ... yaani sisi ni project maalumu ya Mungu kwa ajili ya utukufu wake ...
 
Ndiyo maana Bwana wetu Yesu alikufa pale msalabani, ili ayape maisha maana. Hapo ndipo mauti yake ilikuwa fidia ya kifo cha milele kinachotukabiri sisi wadhambi. Ndiposa,
Siku ya kiyama, ufufuo wake pia umfufue kwa umilele kila aliyeishi duniani akimuamini . Hapo ndipo maisha yatakapotoa maana iliyokusudiwa na Mungu.
Nje ya hapo ni kweli hii kitu haina maana.
 
Furaha ndio kitu kila mtu duniani anatafuta...

So tofauti ni inakuja pale kila mtu anapohisi nini akipata ndio ataipata hio furaha...
Hapo ndipo watu wanatafuta pesa wakiamini itawasaidia kupata wanachokitaka ili wapate furaha
 
Mimi pia naangukia hapo hapo, kifo. Sielewi huyu mgunduzi wetu ana nia gani ya kutuleta hapa, halafu mara puuu, inakuwa kama haukuwahi kuwa hapa!
 
Fuata mafundusho yake na hata ukikosea katika hali ya kibinadamu omba toba
Dada, tunafuata mafundisho, tunasoma maandiko yake, mojawapo linasema, hamna jipya chini ya jua, yanayotokea sasa, yalishawahi kutokea kitambo na yatatokea miaka ijayo. Na zaidi yanasema, maisha ya mwanadamu ni ubatili, ni kama kupuliza upepo! Biblia-Mhubiri.
Hapo unajiuliza nini thamani ya haya maisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…