Hivi TCRA wanadhibiti gharama za matumizi ya mawasiliano ya simu?

KACK

Senior Member
Mar 28, 2015
122
87
Jana nilinunua kifurushi cha internet cha shilingi 500 kupitia mtandao wa Vodacom nikapewa mb 130.

Leo tarehe 24, Januari nimenunua kifurushi cha internet kwa shilingi 500 nikapata mb 70, sijatoka nje ya mkoa wangu.

Mahesabu ya kawaida ni kuwa 130mb - 70 mb = 60mb.

Kwa kutumia hisabati ya shule zetu ni kuwait tarehe 23, Januari mb 1 ilikua na thamani ya shilingi 3.8 wakati tarehe 24 siku moja badae mb 1 inakua na gharama ya tsh 7.1.
7.1tsh - 3.8tsh = 3.3tsh.

What went wrong?
Je, pesa yetu imeshuka thamani?

Je, TCRA mnasimamia na kuhakikisha wanufaika wa mawasiliano kupitia mitandao wanapata haki zao?

Je, kuna utaratibu au muongozo wowote unaoelekeza thamani ya huduma aipatayo mlaji kulingana na kiwango cha pesa kinacholipwa?

Ifike mahala mitandao au mamlaka husika zitujuze kiasi halali cha muda wa maongezi au vifurushi vya internet kwa gharama ya pesa inayotolewa.

Mf:
Tuelezwe mb 1 inauzwa tsh 3 au kuongea kwa simu kwa kutumia mitandao sawa au tofauti kwa sekunde moja ni tsh kadhaa.

Ifike point tutenganishe ofa na uhalisia. Huenda hata mb 70 kwa tsh 500 ni ofa, lakini hatuwezi kujistify hivyo kwasababu hatujui bei halisi na pia baada ya manunuzi hayo unazawadiwa mb za bure.

SUMATRA wanajitahidi kudhibiti nauli kwenye vyombo vya usafirishaji na bei hufahamika kwa wananchi.

Je, TCRA hili wanalisimamiaje?
 
Ukitaka kujua kazi ya TCRA basi muite malaika kale kajina alikopewa na Lissu yaani uchw***

Kwa huu mkurupuko wa kubadilika badilika kwa vifurushi ni dalili tosha hawa jamaa wamelala..
 
Ukitaka kujua kazi ya TCRA basi muite malaika kale kajina alikopewa na Lissu yaani uchw***

Kwa huu mkurupuko wa kubadilika badilika kwa vifurushi ni dalili tosha hawa jamaa wamelala..
Yani kila kukicha pana jipya! Sijui wako sahihi au Mamlaka husika zimefumba macho
 
Wametoa hata kifurush cha kanda ya ziwa. Buku ilkuwa mb 1024.

Watu wameanza hata kupotezana JF. Walishindwa kufungia mitandao ya kijamii sasa wanabana MB
 
TCRA wanafanya kazi kwa UTASHI wa wanaSiasa na sio kwa utashi wa taaluma na ujuzi.
 
Back
Top Bottom