Hivi Tanzania tunaelekea wapi?

Ahmadi Brown

Member
Feb 11, 2019
19
19
#TUJIKUMBUSHE
Ukiambiwa Dr Salim Ahmed Salim aliteuliwa balozi nchini Misri akiwa na miaka 22 halafu ukalinganisha na vijana wetu wa leo wenye elimu na umri huo utaona km vile tunarudi nyuma badala kwenda mbele...

Na ukiambiwa miaka ya 70 hadi 90 nchi yetu ilikuwa na vyama vya ushirika kila mkoa vyenye nguvu kabisa ya kuweza kununua mazao ya wakulima bila matatizo halafu ukalinganisha na Sacco's za sasa hivi za wasomi utaona tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele..

Ukiambiwa zamani nchi yetu bila wasomi ilikuwa na viwanda Mutex mwatex kiltex urafiki nk na mashirika ya umma yenye mafanikio makubwa sana lkn baada ya wasomi kuyaongoza ndo yamefilisika kabisa lazima utakuwa na mashaka na elimu za vijana wetu...

Ukiambiwa zamani kwamba mzazi yeyote alikuwa anaweza kumchapa mtoto ambaye siyo wake na mtoto akienda kulalamika kwao anaongezewa kipigo utajua madili yanazidi kuporomoka kuliko zamani...

Ukiambiwa zamani vijana walikuwa wanachaguliwa wachumba na wazazi wao na wanakubaliana kuoana na ndoa zinadumu tofauti na sasa vijana wanachunguzana miaka mitano lkn wakioana ndoa hazidumu utagundua watu wa zamani hawakuwa na elimu lkn walikuwa na busara kuzidi wa sasa hivi...

Ukiambiwa akina mama wa zamani walikuwa wanaenda shambani na mtoto mgongoni anapitia maji kichwani na kuni lkn wa Siku hizi hata kupika ugali hawawezi utaelewa kuwa Siku hizi wamebaki wanawake majina tu wanatamani kutumia computer kupika wali....

Ukiambiwa zamani wazee wa kimila walikuwa na maadili sana tofauti na viongozi wa dini Siku hizi..utagundua dini zimekuja kwa nia nzuri lkn zinatumiwa vibaya....

Au wewe unaonaje? Kwamba miaka ijayo tutakuwa na wasomi wengi wa mitandaoni lkn watendaji wa mikono hawatakuwepo!
 
Aliyetuloga alishakufa ,Tunaelekea kuzimu bado kidogo tutafika ,UCHUMI UNAANGUKIA KULE MTO WAMI UTALIWA NA MAMBA WALE WENYE UREFU WA MITA 12.
 
Tutafika tu mahali pazuri , hakuna safari ya mafanikio yasiyokuwa na changamoto!
Changamoto zote izo zinakuja kutufanya kufanya makubwa zaidi kuliko apo awali.....worry not
 
Anaye maliza degree umri ni 24, 25, 26 +.. Elimu yetu inapotezea watu mda ikiwa ajira zenyewe siyo uhakika
Hapa kwenye jambo la ajira ni janga kwa taifa kila kona vijana tunalia na serikali. na kwa waliopata ajila nao wanalia mishahara midogo haiendani na elimu walio nayo....so sad
 
Njomba tuko kwenye laiti traki tunaelekea chato... tembea kifua mbele tuko vizuuli!!!
Tusisifie tuu zamani,nako kulikuwa kugumu mmno kiuchumi,kidemokrasia,kijamii,ki mawasiliano,kiafya,ki habari,ki haki za kinamama nk.kwasasa tunamaendeleo tunahitaji tuu kucontrol maadili maana sasa vitu viko hadharani sana ukifanya vyahovyo picha zinasambaa duniani chapu!! No need to blame
 
Back
Top Bottom