Binafsi huwa napata wakati mgumu sana kuelewa maana toka serikali hii ya awamu ya tano iingie madarakani ( I voted for) naona mambo mengi yanafanyika dar tu, sie mikoani ni kama tumetupwa!
Miradi mingi ya kimaendeleo na hata fedha anazotoa mh Rais zinaelekezwa dar tu, vipi kwa mikoa mingine?
Mie ni mkaazi wa kanda ya ziwa, Shinyanga ambapo mh. rais alivuna kura nyingi sana ikiwemo na yangu, kiukweli bado sijaona mema niliyoahidiwa na mh wakati anapita kuniomba kura, kanda ya ziwa vijana wengi wanategemea UCHIMBAJI MDOGOMDOGO WA MADINI KAMA DHAHABU, toka mh ameingia tumefukuzwa kwenye maeneo yetu ya uchimbaji kwa jina la WAWEKEZAJI!
Maisha yamekuwa ni magumu sana kwa sababu kile kidogo tulichokitegemea miaka mingi nacho tumenyanganywa!