Viper
JF-Expert Member
- Dec 21, 2007
- 3,667
- 1,400
...hivi tuna matatizo ya ukomo wa kufikiri?
...mawazo yale yale ya Ubepari ni adui wa haki!
...kwani unalazimishwa ule?
...yale yale,...! target ni kina nani kaka?
...angalau wewe umeangalia nje ya boksi!
..hebu waulize...
...hii ndio athari ya kila kizuri tunasema cha kizungu.
Bandugu mna bore!...
Hivi mnadhani kilio cha serikali watalii/expatriates waje kwa wingi Tanzania maana yake watakula kwa mama Ntilie? au mnataka wale huo ugali na nyama choma mnazozifagilia hapa?
Hamjaweza fikiri MacDonalds watawezesha ajira ngapi hapa nchini? kuanzia wafugaji, wafanyakazi, suppliers, nk? Leo hii hamuoni faida ya Mahoteli ya kitalii, Supermarkets chache tulizonazo, au Mlimani City kwa mfano mdogo?
Hatuwezi kuishi kwa kutarajia mama ntilie atakidhi mahitaji ya watu wote wanaoishi Mijini.
Kwa taarifa yenu, watalii wengi kwenye vigezo vya health & safety hupendelea kula kwenye known/tried and tested franchise kama hizo tajwa hapo awali, ikiwemo KFC, Burger King, Nandos etc, sio kwa mama Ntilie!
Msidhani kuwa kuiga mifumo ya kimagharibi ni dhambi ati tu kwakuwa Mwl Nyerere alisema wao ni makabaila na wanyonyaji! Tumejiingiza kwenye mfumo wa soko huria, lazima twende na matakwa yake.
umeongea nilichotaka niwaambie....