Ndio, Junk Food ni jina(lisilo rasmi) kwa vyakula ambavyo havina virutubisho vya muhimu kwa afya ya binadam,au kama vipo basi vinachanganywa na vitu ambavyo vina madhara katika afya ya mlaji. Haya na wewe unajua maana gani zaidi?
Mkuu, watalii wengi wanakuja kwetu ili waonje vitu tofauti. Ndio mana utawaona wengi wanakwenda sehemu kama Chef's Pride pale mjini n.k. Wewe unafikiri wanalipia ticketi za ndege ili waje kula McDonald's/KFC huku? By the way, wengi wanaofurahia hizo fast food joints huku "ulaya" ni wahamiaji, si wazawa!!!
kama hamtaki macd kwa nini sasa mnakunywa vinywaji kama cocacola?? kwa nini msinywe madude mengine unayoyatengeneza mwenyewe??
tuwekee picha yake hapa..kuna mc d kule kigamboni.
Hakuna chakula mbaya unhealthy kama McD,bora watu waanzishe franchise za vyakula vyetu wenyewe kama ugali,wali na mboga mboga,haya mambo ya mikate na burgers ni vyakula vyao...nafikiri mtalii atafurahi sana akija bongo na kula ugali,maharage na milenda yetu kuliko hizi burger za Mcd!
kwa hiyo wewe kwa nini hutaki macdonald tanzania? kwani ni lazima uende kula??
Haipo maana watakosa biashara. Hawa watanzania wamezoea kunywa uji wa mbege, ndizi nyama, chapati maharage iwe asubhuhi, mchana na jioni. Nashangaa kama watajua jinsi ya kushika hilo liburger la Mcdonald lilivyo likubwa. Basi wanadai ni chakula cha mzungu maana mzungu hali kizito kama mwafrika. Hebu nipe tanoWakuu ningependa kufahamishwa kama Tanzania macdonald ipo na kama haipo kwa nini?
Koba niko pamoja nawe.
Huyo investor wa kula macdonald ndio yale yale ya 'mainvestor' wa kichina waliojaa kariakoo. Investor wa uhakika atakwenda kula sehemu zenye hadhi na sio kwenye junk food.
Kabla ya kushabikia ajira tuangalie pale Subway karibu na office za KLM wana wafanyakazi wangapi? Kuhusu suala la kutumia malighafi zetu kwa wale wanaokula Steers zile juice za unga ni vipi kwani hakuna matunda Tanzania? Je mmewahi kuta kuna Sato au Sangala salad zaidi ya Tuna salad na hizo tuna ni za kopo na ni imported.
Ingekuwa vyema tukashabikia franchise za mtu kama Jamaa Fast Food ambae anatumia malighafi zetu, vyakula salama na bei zake ni more affordable.
Kwani Macdonald kuna nini cha ajabu ndugu zangu hadi inakuwa shida hapa ndani ya jamvi!
Kama itakuja Tanzania ni vema pia ili kwa yule ambae hajawahi kula Macdonald akale na aone tofauti na incase kama haitakuja basi wewe ambaye unaisikia tu usijione kama kuna kitu unakikosa sana mi naukubali sana ugali nyama choma wa bongo kuliko hii MacD.
Kikubwa hapa naona hawa watu waliopo nje ya bongo wanataka waonekani kama wao wanakula vitu vizuri sana kuliko wenzetu kitu ambacho si sahihi hata kidogo.
Misosi ya home ni natural bwana hadi nimeimiss!
haipo maana watakosa biashara. Hawa watanzania wamezoea kunywa uji wa mbege, ndizi nyama, chapati maharage iwe asubhuhi, mchana na jioni. Nashangaa kama watajua jinsi ya kushika hilo liburger la mcdonald lilivyo likubwa. Basi wanadai ni chakula cha mzungu maana mzungu hali kizito kama mwafrika. Hebu nipe tano
kama hamtaki macd kwa nini sasa mnakunywa vinywaji kama cocacola?? kwa nini msinywe madude mengine unayoyatengeneza mwenyewe??
You really dont know what your talking about!!Prevention is better than cure. Kama cocacola ina hizo harmful additives basi isiwe sababu ya kutuongezea more harmful stuff(McDonalds). What we've consumed is enough,what don't need any more of that. Acheni ulimbukeni wa cheap western foods. A person of your age and calibre should feel shy going to fast food joints to eat burger. Eat healthy food,take care of your own body and health. Start now!
...hivi tuna matatizo ya ukomo wa kufikiri?
...mawazo yale yale ya Ubepari ni adui wa haki!
...kwani unalazimishwa ule?
...yale yale,...! target ni kina nani kaka?
...angalau wewe umeangalia nje ya boksi!
..hebu waulize...
...hii ndio athari ya kila kizuri tunasema cha kizungu.
Bandugu mna bore!...
Hivi mnadhani kilio cha serikali watalii/expatriates waje kwa wingi Tanzania maana yake watakula kwa mama Ntilie? au mnataka wale huo ugali na nyama choma mnazozifagilia hapa?
Hamjaweza fikiri MacDonalds watawezesha ajira ngapi hapa nchini? kuanzia wafugaji, wafanyakazi, suppliers, nk? Leo hii hamuoni faida ya Mahoteli ya kitalii, Supermarkets chache tulizonazo, au Mlimani City kwa mfano mdogo?
Hatuwezi kuishi kwa kutarajia mama ntilie atakidhi mahitaji ya watu wote wanaoishi Mijini.
Kwa taarifa yenu, watalii wengi kwenye vigezo vya health & safety hupendelea kula kwenye known/tried and tested franchise kama hizo tajwa hapo awali, ikiwemo KFC, Burger King, Nandos etc, sio kwa mama Ntilie!
Msidhani kuwa kuiga mifumo ya kimagharibi ni dhambi ati tu kwakuwa Mwl Nyerere alisema wao ni makabaila na wanyonyaji! Tumejiingiza kwenye mfumo wa soko huria, lazima twende na matakwa yake.
Yaani MBU- niliposoma hoja zako imebidi nami nijibu thread hii.
Si kweli , uanzishwaji wa MCd, Wendy, KFC, na nyinginezo zitawavutia watalii kuja kwa wingi katika nchi zetu na kula vyakula hivyo. Watalii wengi wanapokwenda kutembelea ughaibuni wanataka kuonja vyakula vya wenyeji, changamoto iliyopo ni kutengeneza vyakula vya kienyeji, katika hali ambayo itavutia wageni, kwa kuzingatia usafi, viwango nk...
Mahali popote duniani , sekta ya utaliii, inavutia wengi kwa jinsi ambavyo wenyeji wameweza kutunza utamaduni wao,vivutio vyao vinavyotambulisha eneo na huo utamaduni ndiyo unawavutia watalii kujifunza,kujaribu ustaraabu au kuushangaa ustarabu huo, kwani hujasikia ukitaka kushangaa nenda feli!!!! Anyway somo la vivutio vya utalii na utalii wa aina gani ni somo pana, ambalo linahitaji muda zaidi.
Tatizo lilipo kwa watanzania wengi, ambao wameenda nje na wanataka kufanya biashara Tanzania, wao huangalia business concept za nje na kuleta hapa kwetu kama copy bila kuzingatia hali halisi ya nchi husika ( local situations) , sikatai kwamba unaweza kufanikiwa kwa njia hizo !!
Lakini ninategemea mtu ambaye ameenda nje na anataka kufanikiwa kikwelikweli na kuleta mguso katika uchumi wa nchi kama Tanzania, aje na wazo mbadala kwa kutumia mazuri aliyoyaona nje, na hapo ndiyo anakuwa amepata elimu ya kupambana na mazingira yake.
Kwa mfano, fast food za kitanzania unavyoweza kuanzisha, ni kupika vyakula vyetu kwa mapishi ya kitanzania,halafu ukatumia business concept za fast food za Ulaya / Marekani, ikiwa unaweza kuweka mfumo ambapo mtu anakuja na gari anaagiza na anapewa chakula,kulipa akiwa kwenye gari. Hapa Tanzania watu wengi sasa wana magari, lakini biashara nyingi, hawafikiri hata kujenga parking lot za kutosha, au kuhudumia watu wakiwa ndani ya magari na vile vile kuhudumia watu watu wasiokuja kwenye biashara yako kwa home delivery nk , nk.
Mtu aliye serious anaweza akafungua franchise yake kwa concept ya kitan zania na akafanikiwa, anahitaji kujua juu ya food quality, to establish a network of reliable food suppliers na kutengeneza mfumo wote mzima.
Jamani nawakilisha kwa sasa, ili na wengine wachangie, lakini WILL BE RIGHT BACK.
kuna spur pia - franchise ya sa..usijali sana haya majina...utamu ni ule ule tu.