Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,900
- 3,206
Tanzania ni mojawapo ya nchi nzuri na ya kuvutia duniani. Inazo raslimali za aina mbalimbali na zingine ambazo huwezi kuzikuta sehemu nyingine duniani.
Kwa ufupi, Tanzania ni moja kati ya nchi tajiri sana duniani, japo watu wake wengi ni maskini wa kutupwa.
Umaskini wa Watanzania umechagizwa kwa sehemu kubwa kutokana na uongozi mbaya wa baadhi ya viongozi wake. Hili ni jambo la kusikitisha sana kwa sababu licha ya upendeleo ambao tumekuwa tunawapa viongozi wetu kuhakikisha wanaishi maisha mazuri wao na familia zao, lakini bado wengi wao wamekuwa wakitulipa mabaya badala ya mema!
Watanzania wengi ni wapole na wasiotaka fujo kwa asili.
Sasa, baadhi ya viongozi wa juu wamekuwa wakilichukulia hili kwa ajili ya kujinufaisha. They have been taking this for granted!
Hii inathibitishwa na changamoto zinazoendelea kwa sasa hapa nchini kwetu. Watanzania wengi hawataki masharti ya hovyo yaliyoko kwenye mkataba wa Kimangungo wa DP World, lakini viongozi wao wa juu wameziba masikio na hawataki kusikia chochote kutoka kwa Raia wao. Halafu wakati wa Kampeni utawaona wanarudi kwa hawa hawa wananchi wanaowapuuza sasa hivi na wengine hufikia hadi hatua ya kuwapigia magoti wananchi ili tu wapate kuchaguliwa, na wakiisha chaguliwa wanawasahau na kuwadharau hao hao wananchi kwa miaka 5 tena!!
Demokrasia ya kweli inatwambia viongozi ni wawakilishi wa wananchi. Na wananchi ndo wanapaswa kuwa na kauli ya mwisho kuhusiana na mambo yanayohusu nchi yao. Lakini kwa sasa Tanzania imekuwa kama nchi ya Kisultani, ambapo viongozi ndo wana kauli ya mwisho kuhusiana na mambo ya nchi!!
Hii haikubaliki kabisa, sasa au baadaye.
Nimalizie kwa kuwaomba sana viongozi makaoupitia huu uzi kwamba, hebu jitahidini kurudisha fadhila kwa Tanzania kutokana na wema ambao Tanzania imekuwa ikiwatendea.
Tafadhalini sana, acheni kabisa kuichezea Tanzania. Kama imewashinda, waachieni wengine waiongoze. Tanzania ina watu zaidi ya Milioni 60. Haiwezi kukosa watu wa kuiongoza.
Tafadhalini sana, tuachieni Tanzania yetu kama mlivyoikuta.
Acheni ubinafsi, acheni ulafi, acheni tamaa.
Kumbukeni, tumeirithi Tanzania ili tuweze kuwarithisha vizazi vyetu.
Mungu ibariki Tanzania pamoja na raslimali zake zote,
AMIN.