Hivi tabia hasa ya wanawake ni ipi?

Hivi tabia hasa ya wanawake ni ipi?

getrusa

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
2,150
Reaction score
1,824
Wakuu nimetafakari jambo hili lakini nashindwa kumuelewa hasa kiumbe aitwae "Mwanamke" Watu hawa katika mahusiano unapoanza kumtongoza unayepata shida ni mtongozaji lakini akisha ingia kwenye mahusiano yeye ndie atakayetaka kumiliki mahusiano hayo.

Akiwa na watoto wake kabla ya ndoa "Mume" unaweza kulea bila kinyongo wala shida lakini, lakini leta wa kwako ulio zaa na mwanamke mwingine kabla ya ndoa wakiishi kwa amani na upendo ni kwa kudra za mwenyezi Mungu,

Ukiwa na fedha ukamuoa yeye hana fedha maisha ni furaha na amani, kinyume chake muoe aliye na fedha kisha wewe kapuku ( maskini) mkiishi kwa furaha na amani ni ngekewa.

Mwanamke akiwa katili katika familia watetezi wa haki za wanawake ni viziwi na vipofu hawataona kamwe na hata wakiona halitakuwa na mashiko katika taasisi zao.

Mwanaume ikitokea kafanya ukatili japo kwa bahati mbaya (hasira) kila taasisi ya wanawake itahusika kulisemea hilo,
Na wale watetezi wa haki za wanawake hapo ndio mahali muafaka kwao kujionesha..

Naomba walio na elimu ya saikolojia ya kijamii wanisaidie kulielewa hili kupitia Uzi huu

Karibuni.
 
Imeandikwa tuishi nao kwa akili.

Inatupasa kumuomba Mungu saana atupe hekima na kuwaombea wenzetu hawa wae na hekima. Mkiwa na hekima na hofu ya Mungu mtaishi kwa amani saana. La sivyo utaona dunia ni kama jehanamu
 
Tabia ya mwanamke ni wewe mwanaume utakavyo mlea

BTW pole kwa kutendwa
Sijatendwa mkuu nimekuwa naangalia tabia ya mamsapu anavyo watendea wasichana wake wa kazi hapa home imenifanya nitafakari mengi sana.!
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] umetisha sana mkuu
Mimi kama mwanamke, umenitoa kwetu Lushoto ukanileta Dar.
Kwahiyo ni jukumu lako kunilisha, kunivesha, kunihudumia, kunipa unyumba (ukizubaa nakucheat), kunipeleka saloon.
Ukiona umeshindwa, ruksa kuniacha
 
We tupe hela tu, hayo mengine huwezi yaelewa.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji23] bahati mbaya pesa haijawahi kuwa na ukomo "kadri unavyopanua ndivyo watu wanavyotamani"!
 
Yes, akitoa zaidi yako nawe unatoa zaidi yake.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji23] bahati mbaya pesa haijawahi kuwa na ukomo "kadri unavyopanua ndivyo watu wanavyotamani"!
 
Mimi kama mwanamke, umenitoa kwetu Lushoto ukanileta Dar.
Kwahiyo ni jukumu lako kunilisha, kunivesha, kunihudumia, kunipa unyumba (ukizubaa nakucheat), kunipeleka saloon.
Ukiona umeshindwa, ruksa kuniacha
Huko kukuacha kwenyewe shughuli yake siyo ya kitoto.! [emoji53][emoji53]
 
Ili umjue vizuri Anna na hii volume one na zipo volume 4
tapatalk_1537264219830.jpeg
 
Back
Top Bottom