Hivi taarifa za hali ya hewa TMA zinaunyeti gani hadi zipatikane kwa wataalamu tu na sio mitandaoni

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Nimemsikiliza meneja utabiri wa TMA na alipoulizwa taarifa zinapatikana wapi anadai ni kwa wataalamu wao mikoani na ukitaka zaidi uende makao makuu dsm.

Mawazo yangu
Hawa watu wanawebsite ambayo inakitengo cha utabiri na ushauri cha ajabu hakuna updates na wwnaweka namba za simu za mezani huku wakijua unyeti wao walipaswa kuweka angalau namba za mitandao yote ili kuwapa unafuu wananchi wenye Nia ya kupata hizi taarifa.

2: mtandao wa viatel umewezesha upatikanaji wa Internet hadi mashambani kwa nini wasiweke online helpdesk au hotchat kwa msaada wa yoyote. Au kuwe na callcenter ambapo wapo 12hrs kama 24 hrs ni ugumu kama kweli wanathamini wakulima hasa wakulima biashara na wale wanalima chakula cha kujikimu.

Kuna haja kama hizi taarifa ni za kutegemewa na kilimo cha mvua bado ni muhimu katika kulitumia eneo lote la tanzania maana tulisoma umwagiliaji sio nchi nzima ni illigable, Kuna umuhimu mkubwa taasisi hii ikawa active kuliko taasisi zote zinazojihusisha na kilimo.
 
Back
Top Bottom