Wakuu wa JF
Nina wasiwasi na Social Security Reguratory Authority (SSRA) kama itakuwa inaitendea haki mifuko mingine maana imehamisha wakurugenzi toka PPF. Tanzania tuna mifuko mingi kama NSSF, PSPF, GEPF, LAPF, NHIF, ZSSF na PPF Fisadi.
Angalia hali ilivyo:
1. Mkurugenzi Mkuu, Katokea PPF kama Investment Manager kapitia Stanbic Bank
2. Mkurugenzi wa Ukaguzi (Director of Internal Audit), Katokea PPF kama Audit manager
3. Director of IT, Katokea PPF kama Director of IT (Huyu ni Mganda)
4. Director of Public Relations, Katokea PPF alikuwa kama PR Manager.
MENGINE:
1. Director of Operations katoka naye Stanbic Bank. Hana hata background ya Social security. Ina maana alikosa kutoka mifuko mingine yote?
2. Juma Mhimbi: Board member alikuwa PPF kama Director of Finance kabla ya kuondolewa kwa ubadhirifu, na bado ana kesi na PCCB. Yupo nje kwa dhamana. Serikari imekosa waadilifu hadi kutumia watu wenye kesi mahakamani? Nasika hata NBAA nao wanamtumia kwenye bodi zao
Mchukia fisadi, kwenye ushindani wa soko la ajira, kinachoangaliwa ni sifa, vigezo na uwezo, maadam hao SSRA walitangaza kazi, wenye sifa wakaomba, hao waliotoka PPF ndio wakawashinda wengine wote, sasa tatizo liko wapi?.
Ikitangazwa kazi ya kutafuta marcernary, watakaoshinda wote watatoka JWTZ, vivyo hivyo, ikitangazwa nafasi ya hansard writers mahali, watakaoshinda wote watatoka bungeni!.
TCRA ni regulatory wa mawasiliano, ilipoanzishwa kazi zilitangazwa, na walioshinda nafasi zote, ni watumishi wa iliyokuwa Tume ya Mawasiliano.
TBC ilipoanzishwa kama TVT, kazi zote zilitangazwa, na wote walioshinda ni waliokuwa wafanyakazi wa AVI na wachache wa TFC.
Maadam SSRA ndio regulatory wa hii mifuko, kazi zilipotangazwa ndio zikawakuta hou wa PPF ndio more qualified kuliko wenzao wa NSSF, PSPF, LAPF na GEPF, if at all nao waliomba kazi.
Naomba kutoa ushuhuda personal kuwa huyu mama mkurugenzi mkuu wa SSRA, hata kama alibebwa kwa gender na beaty yake, lakini ana uwezo, na ameshaonyesha anaweza na hivi karibuni mtaushuhudia uwezo huo!.
Niliwahi kushauri mahali humu humu jukwaani, tufike mahali, tuapunguze kulalamika na badala yake tuchukue hatua!. Kama unaudhibitisho wa upendeleo wa wazi, mbona channel ziko wazi, wide open kuonyesha kuna wazuri zaidi yao wameachwa kwa mizengwe ili hao waliopendelewa wapigwe chini?.
Binafsi niliwahi kajiriwa mahali nikiwa 3rd from top kwenye idara yangu wakati huo nikiwa na just bachelor degree, chini yangu kulikuwa na watu kibao na masters zao, lakini niliwaacha nyuma. Nikapigwa zengwe nikashushwa na nafasi yangu akapewa mmoja wa wenye hizo masters, kilichofuata, alishindwa kudeliver na kutupwa mbali, by that time nami nilishajitambalia zangu kitambo!.
Ndio maana nikakusisitizi kupata kazi fulani, sio sifa tuu, bali vigezo na uwezo. Jee kwenye hiyo safu ya SSRA, hao waliopo wana sifa, vigezo na uwezo?.