Hivi siku hizi PCCB wana mamlaka ya kushtaki?

Wdl

Senior Member
Jun 2, 2017
142
250
Nimeona kesi ya IPTL ( Sethi na Rugemalila) inasimamiwa na PCCB but kwa uelewa wangu. PCCB wanafanya uchunguzi then wanapeleka jalada kwa DPP kwa ajili ya mashtaka je huu utaratibu umebadilika?
 

Hute

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,557
2,000
Nimeona kesi ya IPTL ( Sethi na Rugemalila) inasimamiwa na PCCB but kwa uelewa wangu. PCCB wanafanya uchunguzi then wanapeleka jalada kwa DPP kwa ajili ya mashtaka je huu utaratibu umebadilika?
takukuru wanaweza kupeleka mtu mahakamani ila kwa kutumia wanasheria wao waliopata kibali cha dpp, vilevile kibali cha dpp kwao kuendesha kesi ni lazima. hivyo ni kama wametumwa tu na dpp.

kwa kesi kubwa kama hiyo, wao huwa wanajifanya ni kesi yao lakini wanaenda kwa dpp kuomba wanasheria walio wazoefu (kwasababu wao wanao wasio wazoefu) wawasaidie kuendesha kesi. kwani ni nani alisoma ile hati ya mashitaka jana kwa kina habindar pale kisutu? alikuwa takukuru au wakili wa serikali? waliokuwepo mtujulishe tafadhali.
 

sab

JF-Expert Member
Jan 25, 2013
5,738
2,000
Hata wewe unaweza kushtaki , ilmradi uwe na ushahidi wakutosha
 

Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
4,941
2,000
Nadhani kuna makosa ambayo PCCB wanaweza shitaki moja kwa moja hasa madogo ila mengine watashitaki lakini kwa idhini ya DPP
 

mumburya

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
285
500
Issue ya Nassari iinaweza kukwama hapo kama DPP ndiye mwamuzi wa swala zima la kushtaki.
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
697
1,000
Anaehusika na kufungua mashtaka kwa kesi zote za jinai ni DPP lakini kwa vile DPP hana omnipresence power (kuweza kuwepo kila sehemu kwa mara moja) basi akapewa uwezo wa kuwaruhusu watu wengine kufungua na kuendesha mashauri hayo kwa niaba yake..ndio maana sehemu nyingine (hasa wilayani) kesi zinaendeshwa na waendesha mashtaka wa polisi (maarufu kama PP) na ndio hata hao PCCB wanashtaki baada ya kupewa kibali cha kuendesha mashauri hayo...tofauti ya PCCB na polisi ni kuwa PCCB kibali chao ni kwa shauri waliloliombea kibali tu likiisha inabidi waombe kingine wakati PP akipewa instrument anaendelea kuendesha mpaka pale atakapozuiwa..

So generally DPP ndie anaedeal na kesi zote za jinai
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom