Hivi sheria/taratibu zingine huwa zinawekwa za nini?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi sheria/taratibu zingine huwa zinawekwa za nini??

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Sangarara, May 21, 2012.

 1. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Najua zipo nyingi, leo nitatoa mbili
  KWANZA, Kuna hii ya Cheque inayozidi 10M haiwi processed through BOT clearing house, lakini unakuta mtu anaandika cheque mbili anamlipa mtu yuleyule mmoja, tarehe ile ile, za Milioni Saba Saba, zinaenda BOT na zinapita? Najua BOT wameiga regulation hii kutoka somewhere uko nje? Kwa nini hawakuuliza mantiki yake kabla ya kuja kupest huku kwetu?

  PILI, kuna hii ya kwamba Mgeni haruhusiwi kufungua kampuni hadi awe na shareholder mmoja wa kibongo, ama sivyo kampuni hiyo haitaweza kufungua account Bank. Kampuni inafunguliwa na wamiliki wawili, Patel with Canadian Nationality na Advocate Sangarara with Tanzanian Nationality, Signatory wa Accounts zote za Kampuni ni Mr Patel Peke Yake, Kampuni hii inafungua Bank Account, BOT wanareview na kuendorse kwamba taratibu zote zimefuatwa? hivi hawa Ma Banker wetu wanaelewa mantiki ya kuweka taratibu kama hizi?

  Tujadili.
   
Loading...