hivi serikali ni ya kisanii namna hii au niwatendaji?

drphone

JF-Expert Member
Sep 29, 2009
3,542
281
jamani serikali imetangaza kwamba itagaramia mazishi yote na jana walikuja kwa jirani yetu wakatangaza watatoa sh.1.5m kwa ajili ya kusafirisha na watato mchele na sukari na mafuta hiyo ilikuwa jana jioni wakasema kesho yani leo wangeleta usafiri kwa ajili yakwenda kuchukua mwili wa marehemu kuulete nyumbani kisha kusafirisha.

Mpaka dk hii akuna chochote kilichofanyika wakiulizwa wanasema wapo kwenye msafara wa waziri mkuu.

Watu tumeahamua kuchangisha ili mwili ukachukuliwe na kusafirishwa, hivi serikali inaweza kufanya usanii namna hii jamani?
 
Aisee inaumiza sana.kwa ushauri wangu watakapokuja kuleta hizo fedha mzikatae.
 
Inasikitisha sana na inatia uchungu sana,yaani msafara wa waziri mkuu ni muhimu kuliko kuendelea na misaada ambayo waliahidi ktk kusaidia wafiwa na wagonjwa

Kweli kabisa sasa serikali yetu haitujali kabisa kabisa
 
Nawasihi wale wote waliopoteza jamaa zao huko goms, waendelee na taratibu zao za mazishi wasitarajie kupata msaada kutoka serikalini, kwani yalikuwa ni maneno tu ili tuamini kuwa wanatujali na wameguswa, HAMNA LOLOTE UTAPELI MTUPU.
 
Inasikitisha sana na inatia uchungu sana,yaani msafara wa waziri mkuu ni muhimu kuliko kuendelea na misaada ambayo waliahidi ktk kusaidia wafiwa na wagonjwa

Kweli kabisa sasa serikali yetu haitujali kabisa kabisa

yani tz uhai wa mafisadi ni wa muhimu kuliko watz wote
 
Nawasihi wale wote waliopoteza jamaa zao huko goms,waendelee na taratibu zao za mazishi wasitarajie kupata msaada kutoka serikalini,kwani yalikuwa ni maneno tu ili tuamini kuwa wanatujali na wameguswa,HAMNA LOLOTE UTAPELI MTUPU.

ila usanii huu mpaka lini?
 
Mi naona ni wakati sasa wakuanza kuwapiga mawe kwenye misafara yao, hilo ndio sulihisho na kutuma meseji kuwa tumeshawachoka na wakileta ujinga mwengine ni maanadamano nchi nzima.

Msafara wa Pinda ni Muhimu kuliko mazishi ya ndugu zetu waliouliwa kipumbavu na walinda Ufisadi? Tena isitoshe utakuta Pinda ameenda kwenye ngono.

Aibu gani hii, vile kuitoa kwenye matv na kuandika magazetini kulikuwa ni kutafuta umaarufu?
 
Du! Kumbe ww umelijua leo hilo,yaani hao jamaa ndo zao hizo kupotezea,wanajisemesha ili wapinzani wasipate la kuongea.

Ila ngoja kila ujanja janja una mwisho wake tu! maana hata Mungu anaona.
 
Hiyo habari ya misaada ilikuwa ni kwa ajili ya kuwekwa kwenye kumbukumbu zao tu ili 2015 waeleze namna walivyoonesha kuumizwa na tatizo. kwa serikali hii legelege kila kitu kwao ni siasa tu.

Poleni sana watanzania wenzangu kwa tatizo hili, YANA MWISHO
 
Wangekuwa na huruma wangezuia majanga hayo yanayozuilika. Vinginevyo tuendelee kuumia na kufa mpaka tutakapopata akili na kujua haki zetu.
 
Hivi kuna jambo ambalo Mkwere alishasema likatokea ? Watu wakazike tu hamna ukweli hata chembe
 
Mi naona ni wakati sasa wakuanza kuwapiga mawe kwenye misafara yao, hilo ndio sulihisho na kutuma meseji kuwa tumeshawachoka na wakileta ujinga mwengine ni maanadamano nchi nzima. Msafara wa Pinda ni Muhimu kuliko mazishi ya ndugu zetu waliouliwa kipumbavu na walinda Ufisadi? Tena isitoshe utakuta Pinda ameenda kwenye ngono. Aibu gani hii, vile kuitoa kwenye matv na kuandika magazetini kulikuwa ni kutafuta umaarufu? :mad:

nafikiri kuandamana nchi nzima ndio suluhisho
 
Back
Top Bottom