UMUGHAKA
JF-Expert Member
- Sep 1, 2021
- 2,157
- 10,718
Nisikuchoshe na usinichoshe,tusichoshane.
Serikali hii ya Tanzania inayoongozwa na viongozi ambao kila siku wanapenda kupiga selfie na picha tamu-tamu wawapo mbele ya Kamera,INACHUKIZWA MNO na unafuu wa maisha ya mtanzania,kwa kifupi serikali hii haitaki kuona watanzania wanaishi maisha yenye unafuu.
Wakati nchi nyingine duniani zikipambana kutokomeza hali ngumu kwa wananchi wao,hali ni tofauti kwa Tanzania ambapo viongozi wameendelea kuwanyonya na kuhakikisha mtanzania anakamuliwa vilivyo kiasi kwamba mpaka wahakikishe unywele unatoa maziwa ili yakawashibishe watawala.
Viongozi wa Tanzania wapenda sharubati na makange ya mbuni hawataki kabisa kusikia ishu ya kubana matumizi,kubana matumizi kwao ni kama matusi ya udharirishaji wa mwanamke mbele ya kadamnasi kutakakopelekea uyajutie maisha mpaka unaingia kaburini.
Hakika ukizungumzia ishu ya kubana matumizi kwa viongozi utajuta kuzaliwa Tanzania na utashughulikiwa kisawasawa na ikiwezekana utapewa kesi ya uhujumu uchumi.
Hawa ndiyo viongozi na serikali ya Tanzania inayopenda kusifiwa kwa nderemo na vifijo huku ukipaza sauti "Mama anaupiga mwingiiiiii.....Mama aunaupiga mwingiiiiii".Ukipaza sauti kwa nguvu ikapaa hata ikavuka vimo vya mlima kilimanjaro,nakuhakikishia ya kwamba,hata kama hukusoma wewe jiandae kupokea barua ya uteuzi ya kuwa mmoja wapo wa wanakwaya wa kusifu na kuabudu au almaarufu kwaya ya mtakatifu Mkuu wa Mkoa wa kigango cha Mkuu wa Wilaya.
Jana wakati nikiwa natafakari mambo ya siku itakayofuata,niliamua kuwasha luninga na kutazama taarifa ya habari iliyokuwa ikirushwa na Azam,basi moja ya taarifa iliyonivuta hasa ni habari iliyohusu gesi ya asili ijulikanayo kama Compressed Natural Gas(CNG).
Sasa kikawaida Gas hii imekuwa mkombozi kwa watanzania baadhi wenye magari.
Unafuu wa Gas hii imewapelekea watanzania wengi kubadili mifumo ya magari yao iliyokuwa ikitumia mafuta na kuweka mifumo ya gas hii.
Sasa nilipoitazama ile habari iliyokuwa ya kichunguzi,ilidai kwamba mashine hiyo ya mgandamizo(compressed)ya kujazia hiyo gesi kwenye magari imeharibika kwa muda usiyojulika itatengenezwa au kutengemaa lini,HAKUNA MAJIBU.
Alinukuliwa mwanamama mmoja akisema "kupitia gesi hii kwa siku natumia Tsh 6000/= tu kwenye mizunguko yangu tofauti na hapo awali nilipokuwa nikitumia mafuta ilinibidi kwa siku nitumie Tsh 20,000/=,hivyo hii ni nafuu kuliko mafuta".
Taarifa hiyo ikaendelea kusema,wakati ambapo Lita 1 ya mafuta kwenye gari inayokwenda Km 10,Gas hiyo yenyewe kwa Kg 1 inakwenda umbali wa Km 15,kwasasa Lita 1 ya Petrol inakadiriwa kwa kiwango cha chini kuwa Tsh 2969/= wakati kwa Gas hiyo ikiwa Kg 1 ni Tsh 1550/=.
Sasa kwa mafuta ya Tsh 30,000/=kwa gari ya kutembea Km 101,kwa upande wa Gas hiyo kwa gharama hiyo hiyo gari hutembea kwa Km 290.
Hivyo kwa upande wa wananchi walipata unafuu mno wa maisha.
Sasa kiroja na kituko ni kwamba,inavyoonekana kuna makusudi kutoka katika upande wa viongozi wa serikali ambao hawataki kusikia kabisa unafuu wa maisha ya mtanzania mpaka kufikia kutoa "AMRI" za kuharibu hizo mashine ili watu warudi kwenye mafuta na tozo na makato yaendelee kuchukua nafasi kama kawaida.
Nilitegemea serikali kwa unafuu huu wa Gesi ya asili ungefungua vituo vingi na kuhimiza wawekezaji binafsi wawe wengi ili kuwafanya watanzania wahamasike kukimbia mafuta ambayo yanapanda bei kila kukicha na kuleta unafuu kwa watanzania lakini kwa serikali imekuwa kinyume chake.
Serikali hii haitaki kabisa kusikia unafuu wa maisha kwa mtanzania na haitokaa iruhusu vituo hivi kujengwa kwa wingi kwasababu nia na madhumuni ni kuona mtanzania anakamuliwa vilivyo na kutoa maziwa hata kama hauna vyanzo vya maziwa ni lazima yatatoka utake usitake.
Ishu ya kubana matumizi ya serikali nilitegemea kuona magari mengi ya viongozi wetu ambao wamejivika majoho ya "Miungu watu" yakitumia mfumo huu wa gesi ili kupunguza gharama za mafuta,lakini hili viongozi wapenda starehe na anasa hawataki kabisa kulisikia.
Tumekuwa ni mashuhuda watu wa nchi jirani namna wanavyonufaika na Bandari yetu nzuri ya Dar es salaam,magari yao na mizigo yao inatumia kushushwa kwenye bandari yetu lakini kwa wenzetu kodi zao za magari ni nafuu mno wakati magari hayo hayo yanaposhushwa Tanzania ukisema ulipe kodi mpaka unashika kichwa na kujuta kwanini umenunua,hii imewafanya watanzania wengi kununua mikweche(used cars) kwasababu Serikali haitaki kabisa kusikia unafuu wa maisha kwa mtanzania.
WATANZANIA WENZANGU,SERIKALI HAIPO KWA AJILI YA KUONA UNAPATA UNAFUU WA MAISHA,HIVYO NIKUSHAURI UKATAFUNE NYASI ZA JUNCAO ILI IWE RAHISI KUKAMULIWA UTOE MAZIWA,TOFAUTI NA HAPO UTAENDELEA KUUMIA WAKATI WA UKAMUAJI.
Nawasilisha.