Hivi router nini....?????????

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
554
500
Jaman humu ndani nasoma kitu kinaitwa router afu huwa sielewi sasa wachambuzi wa mambo kinagaubaga mtusaidie sie tunakuwaga njia panda tukisikia maneno hayo.......help plz! !!!!!!!!!!"
 

life is Short

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
4,741
2,000
hii ndiyo router:- ni wireless device kwa mawasiliano ya mtandao,
 

iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,233
2,000
hii ndiyo router:- ni wireless device kwa mawasiliano ya mtandao,
Router siyo lazima iwe wireless. Router inatokana na neno route. Nikifaa ambacho kina ng'amua njia.

HOW.
Mtandao wa internet ni muunganiko wa servers (web servers), nyingi duniani. Mamilioni ya servers. Kila server inakuwa na anwani ya peke yake ambayo inaitwa IP address. Lakini kwa kuwa akili ya binadamu siyo rahisi kushika na kukariri namba za IP address server pia hupewa majina ambayo ni rahisi kushika kwa mfano google.com yahoo.com, utumishi.go.tz etc.

Haya majina ndo tunayotumia ku access servers mbalimbali pale tunapotaka kupata huduma flani.

Servers za internet hutoa huduma mbalimbali ambazo. Huduma huzo hutumia protokali (protocol) tofauti kama vile www, ftp n.k. hivyo unapotaka huduma fulani unatanguliza protocol mfano www.google.com.

kwa sababu computer hazielewi haya majina isipokuwa ip address huitaji huduma nyingine ya zaida kwa ajili ya kutafasiri majina kuwa ip address. Huduma hii hutolewa na server maalumu zinazoitwa dns servers (domain name system servers).

So unapo andika jina la server (domian name) kwenye browser yako kama www.google.com dns server hutafasiri na kutoa ip address ya hiyo server na kuipa router. Router ndo inaangalia njia ya kuifikia hiyo server na kuconnect. Hivyo router zote kwenye internet huwasiliana na kujua njia za kufikia server yoyote iliyoko kwenye internet. Kuwezesha hili router hutunza kumbukumbu iitwayo routing table. Ambayo huijulisha njia ya kufikia server flani. Router hufanya kazi kwa kupasiana na ili uifikie server flani unaweza kupita kwenye router zaidi ya 1 kulingana na server ilipo.

Natumaini maelezo haya mafupi yamekupa mwanga. Kama una swali waweza kuuliza nikufafanulie zaidi.
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,662
2,000
Jaman humu ndani nasoma kitu kinaitwa router afu huwa sielewi sasa wachambuzi wa mambo kinagaubaga mtusaidie sie tunakuwaga njia panda tukisikia maneno hayo.......help plz! !!!!!!!!!!"

Router ni kama mnara wa simu. Kitaalamu zaidi inaitwa Layer 3 Device (kuna layers 1-7 kwenye model ya network data transmission inayoitwa Open System Interconnection Model au kwa kifupi OSI Model). Router ni intelligent device kwa sababu ina uwezio wa ku-route data kwa kutumia IP addresses, in as much as mnara wa simu unavyoweza ku-route information inayotoka kwa A (namba 0713-222) na inatakiwa kwenda kwa B(namba 0713-444), na kweli ikaipeleka kwa B bila ya kukosea kuipeleka tuseme kwa C (0713-666). Na router pia inafanya kazi hivyo hivyo ikitumia IP addresses (ambazo zinafanya kazi sawa na namba za simu), kama vile mnara wa simu unavyotumia namba za simu. Kuna Hub pia ambayo yenyewe iko Layer 2 na haitumii IP addresses, haina uwezo huo, ila pia na yeyewe inaweza kuunganisha Kumpyuta zaidi ya moja na kuziweka kwenye mtandao

Zaidi Router inatumika ku-connect kati yake na Layer 2 Devices kama vile Hub, au moja kwa moja kwenye Layer 1 Device (Kompyuta) kwa kutumia Category 5 Unshielded Twisted Pair (CAT5-UTP) Ethernet Cables. yaani hizi waya za internet unazochomeka kwenye port yako ofisini kwa ajili ya kupata mtandao. Mchoro huo hapo juu wa iMind una maelezo mazuri sana kama tayari uko na knowledge fulani ya haya mambo ya networking. Jaribu kuu-study vizuri!
 

Veyron

JF-Expert Member
Feb 6, 2012
554
500
Mkuuu hapo naomba ushaur kidogo unaweza ukaitumia kuaccses hata katika maeneo ambayo hayana covered ya internet mfano mashambani na ukaweza kupata full access .......halafu huwa zinapatika kwa bei gan?
 

Makanyaga

JF-Expert Member
Sep 28, 2007
5,662
2,000
Mkuuu hapo naomba ushaur kidogo unaweza ukaitumia kuaccses hata katika maeneo ambayo hayana covered ya internet mfano mashambani na ukaweza kupata full access .......halafu huwa zinapatika kwa bei gan?

Kwani ewe hasa unataka kuitumia kuunganisha nini na nini? Router inaunganisha kompyuta zaidi ya moja (Local Area Netwok -LAN), au mtandao tuseme Aitel na wa Vodacom, kusudi kuwe na mawasiliano kati ya watej wa Vodacom na wale wa Aiortel, etc, au Mandao wa Marekani na wa Tanzania -Wide Area Network (WAN).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom