Ki Mun
JF-Expert Member
- Oct 6, 2014
- 3,443
- 4,384
Tweets za Rais Magufuli zimekuwa zikiibua utata mkubwa kutokana na watu kuamini kuwa anachokiandika huwa hakitoki moyoni kwa sababu maandishi yake kwa kiasi kikubwa ni tofauti sana na kauli ama matendo yake...leo tena kaposti kuwatakia Wanawake heri ya siku yao, kinyume kabisa na dhamira yake ya kuwanyima elimu wasichana waliopata ujauzito kuendelea na shule... na wenye akili zao hawakuchelewa kumkumbusha(au kumpa makavu?)
Majuzi pia alizua utata kwa tweet zake juu ya kifo cha mwanafunzi Akwilina aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi, na hata baada ya Lissu kushambuliwa kwa risasi. Sasa mtu unajiuliza, huwa hatafakari kwanza na kurejea kauli zake za nyuma kabla ya ku-tweet? Au hao vijana wake wa press ndo wanamfanyia makusudi?