Andrews,
Ahsante sana kwa swali lako zuri! Lakini niwie radhi kabla sijalijibu nieleze yafuatayo.
Natambua sana ni kwa kiasi gani wasioipenda CCM wanavyonichukia wakiamini kuwa uwepo wangu na juhudi zangu ni sehemu ya vikwazo vikubwa vya hicho wanachokitaka kitokee kwa CCM kutotokea! Hili sina msaada kwao! Hivyo kwa hili nawaruhusu na kwakweli wana haki ya kunitukana watakavyo!Ndo maana pamoja na matusi yote , kejeli zote humu ndani hazinifanye niichukie hii forum au niwachukie wachangiaji kwani wana uhuru wa kusema watakalo. Sana sana ninawazidi ujasiri kwani wao wote wanaotukana hakuna anayethubutu kuingia kwa jina lake halisi, wote wameficha majina yao na ID zao halisi...SITISHWI WALA KUBABAISHWA NA VIVULI VYA WATU!!
Swala la madaktari!!
Sijahoji hata kidogo, wala sitahoji hata kidogo taaluma yoyote acha udaktari, taaluma yeyote hata yako, sihoji!!! Si kazi yangu, wapo waliopewa kazi hiyo!!kama we umechakachua ya kwako basi tuache tuliokaa darasani tukasota mpaka kufika hapa tulipo fika. NIMESOMA HILI SILIONEI HAYA, MAANA NIMESOMA SI KWA KUBAHATISHA, na kwakweli elimu ndio urithi pekee imara alioniachia marehemu babaangu.
Nilichouliza juu ya madaktari, JE HAKUNA NJIA NYINGINE YA KUDAI MASILAHI YAO MPAKA KWA KUWAADHIBU WALIOTOA PESA ZAO KWA NJIA YA KODI WAO WAKASOMA MPAKA KUFIKA HAPO? JE INGEKUWA NI WAZAZI WAO KWA MFANO BABA AU MAMAAKO WAKO TAYARI WAWAFIE MIKONONI KISA KUNA MASILAHI WANADAI KWA SERIKALI??
Naomba ifahamike wazi hapa mimi sipingi wao kudai haki/masilahi zaidi, sipingi hata kidogo, ninachohoji ni njia waliyotumia ndio njia pekee?/
MNAOTAKA TUJADILI KARIBUNI, WALE WA MATUSI NA KEJELI SINA MUDA MCHAFU WA KUWAJIBU.