Kwenye barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliyomwandikia Rais mwanzoni mwa mwaka huu, naona baada ya kuisoma alielewa kipengele kimoja tu: Ya kwamba yeye si mtawala bali Ni mtumishi wa Wananchi. Hii ni kwa sababu siku hizi katika kila jukwaa atakalosimama hakosi kulisisitiza hili.
Lakini Kuna mengi Mhe Rais hakuyaelewa. Mojawapo Ni hili la ubaguzi hasa wa kivyama. Huwezi kutoa amri inayogawa watu katika makundi ya kivyama katika nchi halafu ukadai Wewe Ni mtumishi wa wote. Haiwezekani. Rais hawezi kutumikia mabwana wawaili. Ni lazima atumikie bwana mmoja: Wananchi wa Tanzania.
Sasa Rais anatoa amri inayotugawa Watanzania katika makundi ya vyama leo, kesho atatoa inayotugawa katika dini, na keshokutwa itakuwa ya kutugawa katika makabila. Kama umeamua kutoa amri haramu inayoumiza, ni Bora amri hiyo iwe kwa wote. Ni lazima iwe sawa na msumeno, ilayo kotekote.
Utashangaa akina Bashiru wanashadidia hali hiyo. Bashiru, 'you have to take the bull by its horns.' Tell the Chairman the truth of the matter. That's open segregation!!!