Hivi Polisi wana Taarifa za huu mkutano?

ggenerale

Senior Member
Jan 20, 2018
178
356
Naona mitaa ya mbezi hapa kuna shamra shamra za chama chetu tawala. Zimefana sana.

Ila natamani leo jeshi letu lingetuonesha kuwa Watanganyika wote ni sawa kwa kuleta yale magari vita pendwa ili kuzuia sherehe hizi.

Maana hata Baba Mwenye nyumba alishasema kuwa Polisi wasiwaone Watanzania ni wajinga
20190428_123010~2.jpeg
20190428_122947~2.jpeg
 
Sasa hapo katika kunogesha zaidi, ACT au CDM wangejumuika upande wa pili wa barabara ili kufanya mkutano wa ndani
 
Sasa hapo katika kunogesha zaidi, ACT au CDM wangejumuika upande wa pili wa barabara ili kufanya mkutano wa ndani
Mkuuu hututakiii mema kunavitu vianrukaga juu lakini vinatua kwenye miili ya watu na hakuna anaejua nanikavirusha😜😜
 
Naona mitaa ya mbezi hapa kuna shamra shamra za chama chetu tawala. Zimefana sana.

Ila natamani leo jeshi letu lingetuonesha kuwa Watanganyika wote ni sawa kwa kuleta yale magari vita pendwa ili kuzuia sherehe hizi.

Maana hata Baba Mwenye nyumba alishasema kuwa Polisi wasiwaone Watanzania ni wajinga
View attachment 1083200View attachment 1083201
Wao wenyewe ni wanachama tena hai hakuna tena ccm wala hakuna fala tena
 
Kwenye barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania niliyomwandikia Rais mwanzoni mwa mwaka huu, naona baada ya kuisoma alielewa kipengele kimoja tu: Ya kwamba yeye si mtawala bali Ni mtumishi wa Wananchi. Hii ni kwa sababu siku hizi katika kila jukwaa atakalosimama hakosi kulisisitiza hili.
Lakini Kuna mengi Mhe Rais hakuyaelewa. Mojawapo Ni hili la ubaguzi hasa wa kivyama. Huwezi kutoa amri inayogawa watu katika makundi ya kivyama katika nchi halafu ukadai Wewe Ni mtumishi wa wote. Haiwezekani. Rais hawezi kutumikia mabwana wawaili. Ni lazima atumikie bwana mmoja: Wananchi wa Tanzania.
Sasa Rais anatoa amri inayotugawa Watanzania katika makundi ya vyama leo, kesho atatoa inayotugawa katika dini, na keshokutwa itakuwa ya kutugawa katika makabila. Kama umeamua kutoa amri haramu inayoumiza, ni Bora amri hiyo iwe kwa wote. Ni lazima iwe sawa na msumeno, ilayo kotekote.
Utashangaa akina Bashiru wanashadidia hali hiyo. Bashiru, 'you have to take the bull by its horns.' Tell the Chairman the truth of the matter. That's open segregation!!!
 
'Wanyonge' ndio hawaruhusiwi kufanya mikutano ya siasa wala sherehe, wanatakiwa wakapige kazi ili walipe kodi kisha chama cha mapinduzi na mwenyekiti wao wazitumbue watakavyo.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom