Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,566
- 41,082
Kati ya watu wamekuwa mstari wa mbele kuupigia debe mkataba wa kishenzi wa bandari, kwa upande wa wanahabari, ni bwana Kitenge. Huyu jina lake linajitokeza miongoni mwa wanaotajwa kupokea hongo ili kuusifia mkataba wa hovyo wa bandari. Na muda mwingi amegharamiwa na DP safari zake kwenda huko Dubai.
Katika kila uovu dhidi ya Taifa, ili uweze kufanikiwa, na lazima uwepo usaliti wa ndani. Hivyo haishangazi kuona katika huu uharamia wa kuporwa kwa bandari za Tanganyika, tunao wasaliti wa ndani.
Jana usiku, Kitenge kwenye online blog yake kaweka taarifa eti kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa amepiga marufuku mkutano ulioandaliwa na CHADEMA kuzungumzia uhovyo wa mkataba wa bandari.
Huyu bwana, sijui ni kutokana na kupofushwa, uelewa mdogo au kuna sababu nyingine, hajui hata mamlaka ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Hajui kuwa kuruhusu au kuzuia mikutano ya vyama vya siasa siyo miongoni mwa mamlaka ya msajili wa vyama vya siasa.
Watu wajinga wasiojua sheria, waliopofushwa iwe kwa rushwa, upendeleo au fadhila, tuwapuuze kwa sababu hawajitambui.
Kitenge anahangaika ili sauti za Watanganyika zisisikike, bila shaka kwa nia ya kumridhisha anayemkuwadia kuwa amefanya kazi kubwa na amefanikiwa kuwafanya Watanganyika wote kuwa wajinga, na sasa wanashangilia mkataba wa hovyo.
Makuwadi na mawakala hawatashinda katika vita hii ya kulinda rasilimali za Taifa letu. Watu wema wanaopigania ulinzi wa Taifa letu, hakika watashinda. Twende kwenye mikutano, huu na mingine mingi itakayofanyika, bila ya kujali imeandaliwa na nani, tukaoneshe umoja wetu katika kupambania Utaifa na heshima ya Taifa letu. Tutaendelea kuwakaribisha wawekezaji lakini tutazuia waporaji wa rasilimali zetu.
Tunamwomba Mungu wetu azidi kutuimarisha katika mapambano haya ya kulinda kile ambacho Mungu alitujalia hapa Duniani, kwa maisha yetu na yale ya wale watakaokuja. Na awalaani makuwadi na mawakala wote wa uovu dhidi ya rasilimali za Taifa letu. Tunaomba, laana ya Mungu ikawe juu yao, wana wao na wana wa wana wao.