Hivi Polisi kutukamia na EFD zenu Dar maana yake ni vita ya raia au nini?

KATASAN'KAZA

JF-Expert Member
Jul 24, 2013
3,097
1,352
Sasa natangaza vita ya kufichua maovu ya polis. Jana unyama niliofanyiwa na polisi siwezi kukaa kimya nikawanyamazia.

Ni jana nilitoka hapo nyuma ya kituo cha bucha upande wa kushoto ukiwa unatoka ubungo pale kuna kikanisa na maduka ile naendesha kwenye service road kuelekea ofisi za ifisi ya mtaa sikuvuka popote/kukatiza barabara polisi eti wananisimamisha na kuniambia kwanini naendeshea upande nikawambia hivi mimi nitoke nyumbani kwangu butcher naenda kama mita 300 ofisi za serikali ya mtaa eti nikaendeshe kilomita 3 tatu kuzunguka rombo ndiyo nivuke tena barabara kurudi nilikokuwa niende ofisi za serikali ya mtaa.

Nikauliza swali hivi nyie ata akili ya kawaida hamtumii nitoke kwangu barabara ya mtaa kwenda ofisi ya mtaa ndiyo hiyo service road afu awaniulizi wanaandika tu.

Kiukweli nakiri nilichukia yamkini ningekuwa na siraha km bastola ningewafyeka kwa hasira walizonipatia afu wananitolea majibu ya kejeli eti huyo bwana wenu ( rais) mnamshangilia alipo kataza kupokea posho zetu.

Sasa naapa nitatoa ouvu wa kila polisi nitakaye kutana naye popote iwe ni uzinzi, rushwa, uonevu na ainq yeyote ya mambo yasiyo na maadili maana km nikukamiana kama Bwata na iwe Bwata poor polis lini unamwandikia mtu kosa bila ata kumhoji. Wakati huo huo wanabagua watu kuwatoza faine pale pale zilipita STK tatu na mwanajeshi sijui km wao wako juu ya sheria na walikuwa wanatokea baruti kabisa. Iweje mimi ninayetokea kwangu nasivuki barabara nifanyiwe unyama.
 
Ni kama vita.
Wanatumia hivyo vimachine kutukomoa kabisa.
Jamani susieni service road ya hapo Butcher mtaliwa vichwa mpaka mshangae.Yamekaa kishambenga yapo tayari kuandika fine ili kumeet target yao
 
Hili la efd mashine limeshawaumiza watu wengi, hadi inaonekana kama vile kuendesha gari nchi hii ni usaliti mkubwa.
Hii yote inatokana na kuwafanya polisi traffic kuwa wakusanya kodi wakubwa badala ya kuwa wasimamizi na waelimishaji wa sheria za barabarani. Wanapewa malengo na kutangaza mabillioni wanayokusanya. Ambayo kwa sehemu kubwa ni uonevu.
Si vibaya kuwa wakala wa kukusanya kodi kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Swali la kujiuliza, ni utaratibu gani au ni chombo gani kimeandaliwa Ku regulate matumizi ya efd mashine walizopewa polisi traffic, hawa waliojaa uonevu, chuki, fitina na ubabe. Ili wasizitumie kwa kuwanyanyasa wananchi kwa manufaa yao?. Wahusika waliangalie hili.
 
Back
Top Bottom