Hivi pale TRA kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi pale TRA kuna nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bnhai, Jul 12, 2009.

 1. b

  bnhai JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi nchini kwetu kumekuwa na rushwa za waziwazi sana bila hata chembe ya aibu. Ninakumbuka nilikwenda TRA ile ofisi wanayotoa leseni. kwa bahati mbaya wakati nakabidhi viambatanisho ili niweze kupewa leseni nikasahau cheti cha macho. Yule mama (muhusika) akanirudishia kwa ghadhabu akasema kama hujui waulize wenzako, mmoja akanivuta pembeni akaniambie weka na shs 2000 (juu ya ile ada halisi ya kulipia leseni). Kwakuwa nilikuwa na cheti cha macho nikaambatanisha sikumpa yule mama ile pesa. Ila akaniadhibu indirect kwa kuniweka muda mrefu. Hivi tutafika tunapokusudia?
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kutoka kwenye rushwa itakuwa ngumu sana, japo inawezekana. Hii ni kwa sababu rushwa imekuwa sehemu ya maisha ya watu kiasi kwamba mtu ikitokea (ambayo ni mara chache) akapata huduma bila kudaiwa rushwa na wahusika anashangaa. Kwani kupata huduma bila rushwa imekuwa ni jambo geni. Kumbe utakuta mara nyingine mtu anatoa rushwa yeye mwenyewe hata kabla hajatakiwa kufanya hivyo. Kwa hiyo, kunahitajika mapinduzi ya fikra sambamba na kuwachulia hatua za kisheria wala-rushwa.
   
 3. b

  bnhai JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe kabisa ila kubwa zaidi ni kuandika vyanzo vyote vya rushwa. Hakuna kuoneana haya
   
 4. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Any place where money is involved then their is an opening for corruption. Mifano ndiyo hito TRA, BoT na hata nafasi za kisiasa. What needs to be in place is a system which will reduce corruption as much as possible.
   
 5. b

  bnhai JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,207
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Nadhani siyo system peke yake hata raia. Kwani wote tukigoma kutoa rushwa, hatutahudumiwa? Jeuri ya rushwa wanaipata toka kwa watoaji. Tuwafundishe watumishi kuishi kwa stahili zao. Watu waamue sasa basi wakiona wanadaiwa rushwa wanashout, that can help. Nani pesa yake haimuumi kisa rushwa?
   
Loading...