Kuna upuuzi mtupu hapa. Hakuna majukumu ya kike wala kiume, labda kwenye mambo ya kuzaa TU ambayo kweli kuna ishu za kibaiolojia ndani.
Nani kasema kulipia nyumba ni jukumu la kiume? Wewe unaongea mambo ya utamaduni, na utamaduni unabadilika kila mara.
Nyie wanawake mnataka haki sawa, kumbe nyie ni wanafiki tu. Mnataka haki ya kufanya kazi, lakini ukifika wakati wa kulipia kitu chochote hamtaki kutoa hela, mnataka kuendelea kuchuna wanaume tu.
Zamani wanaume walikuwa na majukumu ya kulipia vitu vingi kwa sababu wanaume ndo walikuwa wanafanya kazi na walikuwa na hela. Kazi ya mwanamke ilikuwa kukaa nyumbani na kuzaa watoto. Basi. Kwa hali hiyo lazima wanaume wawe na majukumu.
Sasa hivi mnadai haki zote. Na mimi na sema ni vizuri tu, nataka usawa kati ya wanaume na wanawake. LAKINI, huwezi kusema unataka usawa halafu bado mnakuwa tegemezi kwa wanaume wenu hata mkiwa na kazi zenu.
Kwa hiyo, chagueni mnataka nini - haki sawa, au kuendelea kuwa housewives mpaka mwisho. Kama mnataka kuwa housewives jitoeni kazini na vyuoni, nendeni kukaa nyumbani, na sisi wanaume tutawalipia kila kitu. Lakini kama mnataka kazi zenu na pesa zenu, ACHENI KUTUCHUNA SISI WANAUME.